Umoja wa Mataifa umesema hibakusha, ambao ni manusura wa mashambulio ya mabomu ya nyuklia huko Nagasaki na Hiroshima nchini Japan wamesalia kuwa viongozi wa amani na udhibiti wa kuenea silaha hizo nchini humo na duniani kwa ujumla.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres aliyepo ziarani nchini Japan amesisitiza azma ya chombo hicho ya kutokomeza matumizi ya silaha za nyuklia duniani.