Je wafahamu vinavyotibua bayonuai?
Muongo wa kurejesha bayonuai umezinduliwa rasmi mwezi huu wa Juni mwaka 2021 kwa lengo la kurekebisha kile ambacho mwanadamu amefanya kuharibu mazingira ya sayari dunia na vile vile kuchukua hatua kuepusha uharibifu. Je nini kinaharibu bayonuai? Lucy Igogo wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIC jijini Dar es salaam nchini Tanzania amezungumza na Clara Makenya, Mwakilishi wa shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP nchini humo. Bi. Makenya anaanza kwa kuelezea chanzo cha muongo huo.
Wanufaika wa Ziwa Victoria Tanzania walalama kina cha maji kuongezeka
Tarehe 5 mwezi huu wa Juni, Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la mazingira, UNEP unazindua muongo wa Umoja wa Mataifa wa mrejesho wa mfumo wa ikolojia ulioharibika.Hii ina maana miaka 10 ya kurejesha hali ya mazingira iwe angani, ardhini au majini. Uzinduzi huu unafanyika kuelekea siku ya mazingira duniani tarehe 5 mwezi huu wa Juni.