Madhara ya COVID-19 kwa watoto ni zaidi ya kuugua, tusipomakinika athari zitadumu nao milele
Ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF imeonya kuwepo kwa ongezeko kubwa la madhara ya janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19 kwa watoto wakati huu ambapo janga hilo linaelekea kuingia mwaka wa pili.