Msumbiji

09 Aprili 2019

Jaridani Aprili 9, 2019 na Assumpta Massoi

-Kampeni ya dharura ya chanjo dhidi ya kipindupindu Msumbiji yawa na mafanikio makubwa.

-Uchumi wa  nchi za Afrika zilizo kusini mwa Afrika wasuasua lakini Kenya na Rwanda kidedea!

Sauti -
12'17"

Msumbiji yahitimisha kampeni ya dharura ya chanjo dhidi ya Kipindupindu

Nchini Msumbiji, Wizara ya afya inakamilisha kampeni ya dharura ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa kipindupindu ambapo hadi sasa wameshafikia watu 745 609 katika wilaya nne zilizokumbwa na kimbunga Idai.

Kampeni ya chanjo ya kipindupindu yaanza Msumbiji.

Shirika la afya duniani WHO, shirikisho la kimataifa la chama cha msalaba mwekundu na mwezi mwekundu IFRC, Madaktari wasio na mipaka MSF na shirika la Save the Children wanaisaidia serikali ya Msumbiji kupitia Wizara ya afya ya Msumbiji  wameanza leo  kusambaza chanjo ya matone ili kudhibiti kipundupindu na  kuwalinda manusura wa kimbunga Idai mjini Beira nchini Msumbiji.

Tafadhali tushikamane na waathirika wa kimbunga Idai:Wataalam UN

Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, hii leo mjini Geneva Uswisi wametoa wito kwa mataifa, mashirika ya kimataifa na sekta binafsi kuonesha mshikamano na nchi za kusini mwa Afrika baada ya kimbinga Idai kuwaua mamia na pia maelfu kubakia bila makazi huku pia kimbunga hicho kikisabab

Sauti -
2'33"

01 April 2019

Katika Jarida la Habari hii leo Grace Kaneiya anakuletea

-Mkutano wa kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya idadi ya watu na maendeleo wang'oa nanga kwa wito wa kuongeza juhudi kutimiza SDGs

Sauti -
13'12"

Tafadhali tushikamane na waathirika wa kimbunga Idai:Wataalam UN

Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, hii leo mjini Geneva Uswisi wametoa wito kwa mataifa, mashirika ya kimataifa na sekta binafsi kuonesha mshikamano na nchi za kusini mwa Afrika baada ya kimbinga Idai kuwaua mamia na pia maelfu kubakia bila makazi huku pia kimbunga hicho kikisababisha hasara ya mabilioni ya fedha.

 

Vifo vya IDAI vinaongezeka , huku mlipuko kipindupindu waongeza hofu Msumbiji:OCHA

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA , idadi ya vifo vilivivyosababishwa na athari za kimbunga Idai nchini Msumbiji imeongezeka na kufikia 493.

FAO yajiandaa kuwasaidia wakulima na wafugaji Msumbiji baada ya IDAI

Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO  limesema linajiandaa kuzisaidia jamii za vijijini zilizoathirika na kimbunga IDAI nchini Msumbiji kufufua kilimo na masuala ya uvuvi.

Athari za IDAI za anika mzigo wa madeni ya siri Msumbiji-UN

Athari za kimbunga Idai kilichoikumba Msumbiji na kwingineko kimeanika hadharani mzigo wa madeni ya siri ambayo hayajalipwa nchini Msumbuji kwa mujibu wa mtalaam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa.

Msumbiji tuko pamoja katika zahma hii ya kimbunga IDAI:Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa antonio Guterres amesema Umoja wa Mataifa na mashirika yake wako bega kwa bega na watu na serikali ya Msumbiji, Malawi na zimbabwe katika kukabiliana na athari za kimbunga Idai kilichokatili maisha ya watu takriban 700 na kuacha uharibifu mkubwa.

Sauti -
3'3"