Msumbiji

Msumbiji ilinde wazee dhidi ya ukatili hususan wakati wa dharura- Mtaalam huru UN

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa aliyeko ziarani Msumbiji amepongeza serikali ya nchi hiyo kwa juhudi zake na dhamira ya kuweka sera na sheria za kuhakikisha wazee wanafurahia haki zao huku akisisitiza utekelezaji unahitajika. Akizingatia hali ya dharura ya sasa kutokana na vimbunga Idai na Kenneth, mtaalamu huyo ametoa wito kwa mamlaka kuhakikisha wazee wanalindwa kutokana na ukatili na unyanyasaji.

Umoja wa Mataifa wahaha kufikisha misaada kwa waathirika wa kimbunga Kenneth

Wahudumu wa misaada ya kibinadamu wamekuwa wakikimbizana kuwafikishia waathirika wa kimbunga Kenneth msaada wa dharura baada ya mvua kusita kwa muda leo asubuhi mjini Pemba nchini Msumbiji.

Sauti -
2'4"

30 Aprili 2019

Jaridani hii leo na Patrick Newman bado tunajikita na kimbunga Kenneth nchini Msumbiji wafanyakazi wa misaada wakihaha kusaidia manusura huku misaada ikisambazwa kwa helikopta. UNCTAD nayo hii leo Katibu Mkuu wake Dkt.

Sauti -
11'46"

Wahudumu wakihaha kuwafikia manusura Pemba, WFP yaanza kusambaza chakula kwa helikopta hii leo

Wahudumu wa misaada ya kibinadamu wamekuwa wakikimbizana kuwafikishia waathirika wa kimbunga Kenneth msaada wa dharura baada ya mvua kusita kwa muda leo asubuhi mjini Pemba nchini Msumbiji.

UN yatoa dola milioni 13 kwa waathirika wa Kenneth Msumbiji, watu 38 wapoteza maisha

Fedha za msaada zilizotolewa na Umoja wa Mataifa zitasaidia kuhakikisha chakula , malazi, huduma za afya na maji safi vinapatikana kwa waathirika wa kimbunga Kenneth nchini Msumbiji. Nchi hiyo ina watu 18,000 waliotawanywa na kimbunga Kenneth ambao hivi sasa wanapata hifadhi kwenye makazi ya muda. Watu38 wamefariki dunia kufuatia kimbunga hicho kufikia sasa.

Watoto 368,000 wako hatarini Msumbiji baada ya kimbunga Kenneth:UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF limeonya kwamba watoto na familia zao nchini Msumbiji wanaweza kukabiliwa na hatari ya kifo kutokana na mafuriko makubwa na maporomoko ya udongo baada ya shirika la Umoja wa Mataifa la utabiri wa hali ya hewa WMO kuonya kwamba mvua kubwa itaendelea kunyesha. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anatarajiwa kuzuru hivi karibuni nchini humo.

Baada ya kasi ya kimbunga Kenneth kupungua sasa ni mipango ya usaidizi:UN

Baada ya kimbunga Kenneth kupiga jimbo la Cabo Delgado kaskazini mwa Msumbiji jana jioni, na sasa kuwa kimepungua kasi yake, Umoja wa Mataifa umechukua hatua ya kupeleka timu yake ili kusaidiana na serikali katika operesheni za usaidizi na usimamizi wa taarifa.

Sauti -
2'27"

26 Aprili 2019

Jaridani leoni makala kwa kina tukimulika mahojiano na John Jackson ambaye anafundisha lugha ya Kiswahili nchini Ujerumani na ambaye kwa sasa anazungumzwa sana sanjari na mtoto Braydon Bent, mchambuzi wa soka, pengine mwenye umri mdogo zaidi barani Ulaya.  Katika mazungumzo haya John Jackson anan

Sauti -
9'58"

Kasi ya Kenneth Msumbiji yapungua, UN yajipanga kusaidia waathirika

Baada ya kimbunga Kenneth kupiga jimbo la Cabo Delgado kaskazini mwa Msumbiji jana jioni, na sasa kuwa kimepungua kasi yake, Umoja wa Mataifa umechukua hatua ya kupeleka timu yake ili kusaidiana na serikali katika operesheni za usaidizi na usimamizi wa taarifa.

Kimbunga Kenneth kikitarajiwa Msumbiji, UN imejiandaa kuchukua hatua

Kimbunga Kenneth kikitarajiwa kupiga maeneo ya kaskazini mwa Msumbiji jioni ya leo siku ya Alhamisi, Umoja wa Mataifa nchini humo umesema tayari umeanza kuchukua hatua ili kupunguza madhara ya kimbunga hicho ambacho pia kinatarajiwa kupiga maeneo ya kusini mwa Tanzania.

Sauti -
1'52"