msaada wa chakula

Machafuko kaskazini-mashariki mwa Syria ni "mwiba" kwa wenye ulemavu

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP linasikitishwa sana na usalama wa raia walioko katika miji ya RAqqa na Hasake kaskazini-mashariki mwa Syria ambako operesheni za kijeshi zinaendeshwa tangu tarehe 9 mwezi huu wa Oktoba.

WFP yafikiria kusitisha utoaji misaada sehemu zinazodhibitiwa na Houthi nchini Yemen

Shirika la mpango wa chakula dunia WFP linataka mambo matatu ya dharura kufanyika nchini Yemen yakiwemo: uhuru wa kuhudumu, kuwafikia wale walio na njaa na kufanyika usajili wa kieletroniki.

Zaidi ya nusu ya watu Gaza kukosa chakula ifikapo Juni:UNRWA

Zaidi ya watu milioni moja sawa na nusu ya watu wote Gaza huenda wasiwe na mlo kabisa ifikapo mwezi Juni mwaka huu limeonya shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA.

WFP yafanikiwa kufikia kinu cha kusaga nafaka cha bahari ya Shamu Yemen

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP na timu ndogo ya mafundi  wa kampuni ya kusaga nafaka ya bahari ya Shamu ambayo ni muhimu katika usambazaji wa chakula kwa mamilioni ya watu nchini humo, wamefanikiwa kufikakwenye kinu hicho mwishoni mwa juma na sasa wanaendelea na shughuli ya kusafisha na kukarabati mitambo au mashine kwa ajili ya maandalizi ya kuanza kusaga tena ngano na kusambaza kwa wahitaji.

Watu milioni 10 DPRK wanakabiliwa na uhaba wa chakula:WFP/FAO

Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo kuhusu tathimini ya chakula kwenye Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Korea au DPRK imebaini hali ya kutia hofu ya watu kula chakula kidogo, kutokuwa na lishe inayostahilina familia nyingi kulazimika kupunguza idadi ya milo au kula kidogo sana.

Shehena ya kwanza ya chakula yawasili Hodeidah tangu Mei 2018-WFP

Baada ya miezi ya ushawishi na kubembeleza , meli ya MV Elena  imekamilisha kupakua shehena ya msaada wa kibinadamu kwenye bandari ya Hodeidah ikiwa ni meli ya kwanza iliyoshoheni msaada wa shirika la mpoango wa chakula duniani WFP kuwasili bandari hiyo tangu Mei 2018.