Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Monsoon

06 SEPTEMBA 2022

Katika Jarida la mada kwa kina hii leo Flora Nducha anakuletea

-Mashirika ya misaada ya kibinadamu yamesema Somalia imefikia kkatika hali mbayá sana. Maisha ya mamia ya maelfu ya watu yamo hatarini hivi sasa kutokana na tathimini iliyofanywa hivi karibuni kuhusu uhakika wa chakula na lishe. Baa la njaa linajitokeza katika wilaya za Baidoa na Burkhakaba kwenye jimbo la Bay lina uwezekano wa kudumu hadi Machi 2023 ikiwa msaada wa kibinadamu hautaongezwa kwa kiasi kikubwa na mara moja.

Sauti
11'51"
UNHCR/Caroline Gluck

Makazi mbadala kwa warohingya yakamilika- UN

Mashirika ya misaada ya kibinadamu yanayotoa huduma kwenye kambi za wakimbizi wa Rohingya nchini Bangladesh , leo yamekamilisha maandalizi ya eneo la kwanza jipya kwa ajili ya kuhamishia familia za wakimbizi walio katika hatari ya maporomoko yatakayosababishwa na pepo za monsuni.

Sauti
1'42"
© UNHCR/Caroline Gluck

Warohingya wajindaa kabla ya hatari ya monsuni

Nchini Bangladesh shirika la mpango wa chakula duniani, WFP linashirikiana na warohingya waliosaka hifadhi humo katika kuandaa vema makazi na kuhifadhi wa chakula wakati huu ambapo msimu wa pepo za monsuni unabisha hodi.

SFX: watotomaji

Katika makazi ya warohingya huko Cox’s Bazar tayari mvua zilizonyesha zimetwamisha maji ambayo watoto wamegeuza kuwa ni mchezo.

Hali ya mazingira ni duni na WFP ina hofu hali ya mazingira na chakula itakuwa mbaya zaidi mvua za monsuni zitakapoanza rasmi.

Sauti
1'46"
© UNHCR / Andrew McConnell

Mafuriko na maporomo kufuatia Cox’s Bazaar yahatarisha maisha ya watoto warohingya

Watoto 55,000 wanakadiriwa kuwa katika hatari kubwa ya mafuriko na maporomoko ya udongo kwenye makazi ya wakimbizi wa Rohingya nchini Bangladesh limeonya leo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF. 

Japo msimu rasmi wa mvua na pepo za Munsoon haujaanza ,Kwa mujibu wa UNICEF mvua za awali zimeanza na kuleta athari kwenye makazi hayo ya Cox’s Bazaar eneo linalotambulikwa kwa kukumbwa na mafuriko kila mara.

Sauti
1'7"