Mradi wa PLEAD wawezesha huduma za mahamaka kupatikana muda wote nchini Kenya
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya madawa na uhalifu UNDOC kanda ya Afrika Mashariki kwa kushirikiana na sekta ya mahakama nchini kenya wamepanga kuanza kutekeleza awamu ya pili ya mradi wa uwekaji umeme wa sola katika mahakama na magereza nchini humo baada ya awamu ya kwanza kuonesha mafanikio.
Kupitia mradi ujulikanao kama PLEAD unaofadhiliwa na Muungano wa Ulaya UNODC na sekta ya mahakama nchini Kenya wamefanikiwa kutekeleza mradi wa awamu ya kwanza katika mahakama mbili zilizoko Mombasa ambazo zilikuwa zikishindwa kuendesha shughuli zake pindi umeme unapokatika.