SDGs zahitaji kuelewa ndipo zitekelezeke:Muzenda
Ikiwa imesalia miaka 11 kuelekea mwaka 2030 ambao ndiyo umepangwa na Umoja wa Mataifa kuwa mwaka ambao malengo ya maendeleo endelevu, SDGs yatakuwa yametimizwa, Umoja wa Mataifa na wadau mbalimbali wameendelea kuhamasisha umma kwanza kuyafahamu malengo yenyewe na pia kuyatekeleza. Miongoni mwa wadau hao ni Munyaradzi Muzenda kutoka Zimbabwe ambaye ni mkurugenzi wa taasisi ya Africa Speaks, yeye anaendesha kampeni ya kukuza uelewa kuhusu SDGs, Arnold Kayanda na maelezo zaidi.