mkimbizi

Mkimbizi asema vita vikiisha Syria, nitarejea na kufungua duka la mikate ya kijerumani

Nchini Ujerumani, mmiliki mmoja wa duka la kuoka mikate ameleta matumaini kwa vijana wakimbizi ambao awali walihisi maisha yao yametumbukia nyongo kutokana na changamoto walizokuwa wanakumbana nazo ikiwemo lugha na fursa za kujiendeleza. 

Sauti -
2'30"

Mkimbizi bila elimu ni sawa na mti bila matunda:Mkimbizi Rachel

Elimu kwa mkimbizi ni muhimu sana, kwani bila elimu huwezi fanya chochote , iwe ni kwa upande wa ajira au hata ujasiriliamali, unakuwa sawa na mti usiozaa matunda ambao huonekana kutokuwa na faida yoyote.

Sauti -
3'32"

Ukosefu wa amani DRC ni kidonda moyoni mwangu-mkimbizi Lubunga

Mpango wa shirika la wakimbizi duniani, UNHCR wa kuwapatia wakimbizi walioko Tanzania hifadih katika nchi ya tatu umeendelea kuleta tija kwa wakimbizi wakiwemo wale kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambao sasa wanapazia jinsi walivyonufaika. 

Kitendo cha Zambia kumrejesha kinguvu nyumbani mwanasiasa hakikubaliki-UNHCR

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR limesema lina wasiwasi mkubwa kuhusu taarifa za kurejeshwa nyumbani kinguvu kwa raia mmoja wa Zimbabwe aliyekuwa anasaka hifadhi Zambia.

Ndoto zilizoingia katika mashaka ukimbzini, Uganda.

Vijana  ndio nguzo za kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs, kwani ndio viongozi wa sasa na  wa hapo baadaye. Lakini wengi wanakabiliwa na  changamoto za kuweza kufanya vitu ambavyo vitawafaa hapo baadaye. Hali ya vijana katika mataifa yanayaoinukia ni ya shida mno.

Sauti -
3'45"

20 Julai 2018

Jarida na Flora Nducha. La leo limesheni masuala ya wakimbizi; Wa kutoka Eritrea wajumuishwa na jamii Ureno; huduma za kiafya kwao zaimarika.Mkimbizi msanii chupukizi kimuziki kutoka DRC amwaga vyake Uganda , na je wajua maana nagapi ya neno KITANDA? 

Sauti -
11'37"

Wakimbizi si maadui, ni watu wa kawaida waliokimbia kwao kutokana na taabu- Mariella

Shida inapobisha hodi mara nyingi binadamu hukata tamaa na kuamini kuwa huo ndio mwisho wa maisha  yake. Ingawa hiyo kwa wengine kukata tamaa ni mwiko kwa kuwa wanaamini kuwa mlango mmoja ukifungwa, mingine mingi hufunguka.

Sauti -
4'13"

Familia yangu ipo salama: Bi. Marai

Baada ya kupoteza kila  kila kitu wakati wa  migogoro wa kivita nchini kwao Burundi , mwanamke mkimbizi aliyekimbilia Rwanda  anasema , hajutii mali na vitu alivyovipoteza  kwani yeye na familia yake wapo salama aliko ukimbizini.

Sauti -
1'24"

Furahia ya leo kwani ya kesho ajuaye mola

Maisha yana kupanda na kushuka! Ni maneno ya wahenga wakimaanisha kuwa mara nyingine maisha  yanakuwa mazuri na baadaye kutwama. Hivyo ndivyo ilivyokuwa mwa  Tareq Sweidan, raia wa Syria ambaye sasa anaishi ukimbizini nchini Misri! Umaarufu ulimporomoka, kisa? Vita nchini mwao. Je sasa hali iko vipi? Selina Jerobon katika Makala hii anamfuatilia Tareq.

Sauti -
3'40"

Kutoka Nigeria hadi Hungary, kulikoni?

Ama kweli wahenga walinena kuwa mchumia juani, hulia kivulini na methali hiyo imedhihirika kwa raia mmoja wa Nigeria ambaye baada ya kupitia machungu mengi kwenye mikono ya wasafirishaji haramu, sasa ametulia tuli. Ndoto yake ya kufika Ulaya ilitimia na sasa ana ndoto kubwa zaidi.

Sauti -