mkataba wa paris

Uhifadhi wa tabianchi wazidi kupigiwa chepuo

Mataifa yaliyoendelea yameungana na nchi zingine kuahidi kuweka malengo thabiti zaidi ili kupunguza hewa chafuzi kabla ya mwaka 2020.

Mabadiliko ya tabianchi yaleta zahma kwa mamilioni 2017:UN

Mwaka wa 2017 umeelezwa kama ulioshudia matukio yaliyofurutu ada ya hali ya hewa na hivyo kuwafanya mamilioni ya watu duniani kuteseka. Hivyo Umoja wa Mataifa unasema si hadhithi tena bali athari za mabadiliko ya tabia nchi zimeanza kushudiwa hususan katika jamii zilizo hatarini zaidi.

Bloomberg atoa dola milioni 4.5 kupambana na mabadiliko ya Tabianchi-UN

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa, kuhusu mabadiliko ya tabianchi,Michael Bloomberg, ametangaza kutoa dau la  dola milioni 4.5 kwenda kwa fuko la  Umoja wa Mataifa linalohusika na  nabadiliko ya tabianchi UNFCCC.

Ushahidi gani zaidi wahitajika kuamini mabadiliko ya tabianchi yapo?

Watu 900,00 barani Afrika wamekimbia makazi yao kutokana na ukame. Nchi za kusini mwa Asia zimeshuhudia mafuriko makubwa yaliyoathiri awtu milioni 41. Gharama za kiuchumi kutokana na majanga yatokanayo na mabadiliko ya tabianchi ni dola bilioni 320. Hii imevunja rekodi!

Sauti -
1'47"

Utunzaji misitu ni jawabu la mabadiliko ya tabianchi

Utunzaji misitu ni jawabu la mabadiliko ya tabianchi

Mkataba wa Paris kuhusu  mabadiliko ya tabianchi unaziasa serikali, mashirika ya kimataifa na asasi za kiraia duniani kote kuongeza jitihada  katika zoezi la kulinda mazingira.

Sauti -

Mwaka mmoja wa mkataba wa Paris, mafanikio ni dhahiri

Mwaka mmoja wa mkataba wa Paris, mafanikio ni dhahiri

Mkutano wenye lengo la kuchagiza utekelezaji wa mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi utafanyika kesho mjini Paris, Ufaransa, ukienda sambamba na maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kutiwa saini kwa nyaraka hiyo.

Sauti -