minusma

Licha ya purukushani, uchaguzi wafanyika kwa amani Mali

Nchini Mali uchaguzi wa rais umefanyika kwa amani licha ya kuripotiwa kwa visa vya hapa na pale vilivyokwamisha upigaji kura kufanyika katika baadhi ya vituo.

Heko Mali kwa kampeni tulivu, kesho chagueni rais kwa amani- UN

Kuelekea uchaguzi wa rais nchini  Mali hapo kesho Agosti 29, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Gutereres amesema anatiwa moyo na jinsi ambavyo kumekuwepo na amani wakati wa kampeni licha ya changamoto za usalama kwenye maeneo ya kaskazini na kati mwa taifa hilo la Mali.

Machafuko yenye mlengo wa kijamii Mopti Mali yatutia hofu:UN

Machafuko yenye mwelekeo wa kijamii yanayoendelea katika jimbo la Mopti katikati mwa nchi ya Mali yanatia wasiwasi mkubwa kwa mujibu wa ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa.

Sauti -
1'23"

Machafuko yenye mlengo wa kijamii Mopti Mali yatutia hofu:UN

Machafuko yenye mwelekeo wa kijamii yanayoendelea katika jimbo la Mopti katikati mwa nchi ya Mali yanatia wasiwasi mkubwa kwa mujibu wa ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa.

Walinda amani wa MINUSMA watunzwa medali za UN

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ametumia siku yake nzima leo na walinda amani wa ujumbe wa umoja huo mjini Bamako nchini Mali, MINUSMA ambapo amewatunza medali walinda amani wawili wa ujumbe huo.

29 Mei 2018

Jarida hii leo katika siku ya walinda amani wa UN Assumpta Massoi anakuletea:

Sauti -
11'20"

UN inahusu amani na penye amani pana maendeleo- Amodu

Leo ni siku ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa, UN ikilenga kutambua mchango wa wanawake na wanaume zaidi ya milioni moja waliohudumu kama walinda amani wa chombo hicho tangu kuanzishwa kwa operesheni hizo miaka 70 iliyopita. Siraj Kalyango na maelezo zaidi.

Sauti -
1'56"

Mkuu wa UM yuko Mali kuadhimisha siku ya walinda amani

Katika mkesha wa siku ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa kesho Jumanne, polisi wa Mali wanajiandaa kwa doria za usiku kwenye barabara za mji mkuu Bamako kwa kushirikiana na walinda amani wa umoja huo

Mwanamke wa kwanza rubani wa ndege Umoja wa Mataifa ( MINUSMA)

Siku hizi hakuna kazi ya mwanamke wala mwanaume kama ilivyokuwa siku za nyumba mfano kazi ya urubani kwa miaka mingi imekuwa ikifanywa na wanaume lakini sasa wanawake zaidi na zaidi wanaingia katika anga hizo

Sauti -
1'51"

Mwanamke pekee rubani MINUSMA

Huyu ni Sandra Hernandez Vega, raia wa El Salvador ambaye ni rubani wa helikopta ya vita. Anasema ni Imani yake kuwa  kupitia kazi yake anachangia mchakato wa amani na utulivu nchini Mali.