UNESCO yasema uhamasishaji wa kimataifa ni muhimu ili kulinda mikoko duniani
Muda unayoyoma wa kulinda mikoko duniani ambayo sio tu makazi ya viumbe wengi lakini pia ni muhimu dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi, amesema Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Audrey Azoulay, hii leo.