Chuja:

Mifuko ya plastiki

24 Julai 2019

Katika Jarida la Habari hii leo arnold Kayanda anakuletea 

-Mikoko yaleta nuru kwa wakazi wa Pwani ya kenya licha ya kuhifadhi mazingira kwa kupunguza hewa ukaa yawaletea kipato wananchi kwa mujibu wa UN Environment

-Vijana nchini Tanzania wakumbatia mabadiliko ya kuachana na matumizi ya mifuko ya plastiki na kujipatia kipato kwa kutengeneza mifuko mbadala ya karatasi

-Elimu katika shule 25 nchini Kenya yapigwa jeki na mradi wa UNICEF wa  vitabu mtandaoni na matumizi ya Ipad

Sauti
13'35"
Saeed Rashid

Taka za plastiki sio tu uchafu bali ni gharama- January Makamba

Changamoto za taka za plastiki sio tu katika uchafuzi wa mazingira na athari kwa afya za binadamu, bali pia ni gharama kubwa kuzikusanya na kuzitokomeza ikiwemo mifuko ya plastilki. Umoja wa Mataifa unasema ili kufanikisha ajenda ya mwaka 2030 ya maendeleo endelevu au SDGs hasa katika kulinda na kuhifadhi mazingira taka za plastiki ni lazima zikomeshwe. Tanzania miongoni mwa nchi wanachama zinazochukua hatua za kutimiza wito huo na imeanza kutekeleza rasmi sheria ya kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki mwishoni mwa wiki Juni Mosi .

Sauti
4'16"