Michel Sidibé

Kasi ya kudhibiti UKIMWI imepungua- UNAIDS

Kanda zote ziko nyuma katika kudhibiti kuenea kwa Ukimwi na mafanikio makubwa tuliyopata kwa watoto hayahifadhiwi huku wanawake ndio wanaoathirika zaidi, amesema Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia UKIMWI-UNAIDS, Michel Sidibe, wakati wa uzinduzi wa   ripoti mpya ya hali ya UKIMWI duniani hii leo.

UNAIDS yashuhudia jinsi ufalme wa Bunyoro unavyokabiliana na UKIMWI

Ufalme wa Bunyoro umepiga hatua kubwa katika vita dhidi ya ukimwi , lakini pia umejinyakulia sifa kemkem kutoka kwa mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ukimwi UNAIDS, Bwana Michel Sidibe ambaye yuko ziarani nchini Uganda, kwa kudumisha utu wa kuwapokea wakimbizi lukuki wengi kutoka Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.

Sauti -
1'44"

Heko Bunyoro kwa kupambana na UKIMWI-UNAIDS

Mfalme Iguru wa Pili, wa Bunyoro Kitara nchini Uganda  anasifika sana kwa kitendo chake cha kila wakati kutumia hotuba zake kuhamasisha watu wake kujikinga dhidi ya UKIMWI na hii imezaa matunda hadi kupatiwa pongezi na Umoja wa Mataifa.