Mazingira

Mazingira yamefanya familia yangu ipate lishe bora na kipato-Mfugaji wa Sungura Tanzania

Bi Joyce Ballo wa Ifakara Morogoro Tanzania, anasema uamuzi wa wakulima wa mbogamboga na miti katika eneo lake wa kutumia njia mbadala za kutunza mazingira kwa kuamua kutotumia dawa na mbolea zenye sumu, kumempa fursa ya kupata kipato na lishe kwa familia yake. 

 

Sauti -
3'36"

Magari mengi yanayopelekwa katika nchi za uchumi mdogo hayafai-Utafiti

Mamilioni ya magari yaliyokwisha kutumiwa, ambayo yameuzwa katika nchi zinazoendelea, hayafai, yana ubora wa chini na yanachangia kwa kiasi kikubwa katika uchafuzi wa hewa na hivyo kutatiza juhudi za kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi, imesema ripoti mpya ya Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP.