Mazingira

Plastiki ni fursa ya kipato kwa kijana Tanzania

Katika juhudi za kuhakikisha uhifadhi wa mazingira  serikali, kampuni na hata watu binafsi wanachukua hatua katika kurekebisha makosa ambayo yanasababisha uharibifu wa mazingira. Uwepo wa plastiki zinazotupwa kiholela ni moja ya kero kubwa lakini pia athari zake kwa mazingira ni mbaya kwani husababisha changamoto nyingi ikiwemo mafuriko. Katika kuelekea siku ya mazingira duniani kesho Juni 5, tunaelekea nchini Tanzania ambako Tumaini Anatory wa radio washirika Karagwe FM mkoani Kagera anaangazia kijana ambaye amegeuza taka hizo kuwa kiini cha kipato chake.

Sauti -
3'42"

Juhudi dhidi ya matumizi ya plastiki zitumikazo mara moja zapamba moto

Ulimwengu unahitaji ufumbuzi mbadala dhidi ya  matumizi ya vifaa vya plastiki vinavyotumika mara moja na kutupwa.

WHO na WMO kudhibiti athari za kiafya na hali ya hewa

Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa yamekubaliana kuanzisha  mkakati maalum wa pamoja utakaosaidia kudhibiti athari za kiafya zinazosababishwa na mazingira duni.

Je wanavijiji watamudu nishati mbadala ili kulinda misitu Tanzania?

Katika jitihada za pamoja za Umoja wa Mataifa  na serikali duniani kuhakikisha misitu inalindwa ili kudhibiti mabadiliko ya tabianchi, Tanzania imejiwekea mkakati kabambe wa  miaka 5 kwenda sanjari na lengo hilo.

Utumiapo mara moja kijiko cha plastiki na kukitupa wajua kinapoishia?

Baada ya kushiriki na kufanikisha mafanikio ya kampeni ya kutokomeza matumizi ya mifuko ya plastiki nchini Kenya, mwanaharakati na mpiga picha nchini humo James Waikibia amesema hivi sasa ameelekeza nguvu zake kwenye kutokomeza matumizi ya vifaa vya plastiki vinavyotumika mara moja na kutupwa.

Ajira milioni 24 kubuniwa duniani ifikapo 2030-ILO.

Ikiwa sera sawa za kukuza uchumi unaojali mazingira zitazingatiwa  ifikapo mwaka wa 2030, ajira takriban milioni 24 zitabuniwa.

Tanzania yavalia njuga uhifadhi wa misitu

Tanzania imesema inasimamia kidete suala la uhifadhi wa misitu.

Watoto Kenya nao wahifadhi mazingira

Serikali ya Kenya inaendesha  kampeni ya uhifadhi wa mazingira, ambapo elimu ya upandaji miti inatolewa katika shule za msingi ili kuelimisha vijana na jamii kwa ujumla kuhusu umuhimu wa  manzingira.

Sauti -
3'8"

Dawa mujarabu kudhibiti uchafuzi wa mazingira Lagos yapatikana

Ajenda ya 203 ya maendeleo endelevu au SDGs  inazihimiza serikali, asasi za kiraia na kila mwenye fursa kupiga vita uchafuzi wa mazingira na kudhibiti  hewa ukaa itokanayo na maendeleo ya viwanda. Nchini Nigeria katika mji wa Lagos, ukuaji wa mji huo utokanao na maendeleo hususani ya viwanda, imekua kikwazo katika kampeni ya Umoja wa Mataifa ya kupiga vita uchafuzi wa mazingira.

Sauti -
4'12"

Kuhifadhi na kupanua wigo wa misitu ni mtihani tunaotakiwa kushinda:FAO

Idadi ya watu ikiendelea kuongezeka duniani na kutarajiwa kufikia bilioni 9 mwaka 2050, kuhifadhi na kupanua wigo wa mistu kwa ajili ya kuwezesha kuwalisha watu hawa imekuwa mtihani ambao dunia inapaswa kuushinda kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa .