Mazingira

Mnaosuasua kutekeleza mkataba wa Paris tazameni India- Guterres

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi ameibuka mshindi wa tuzo ya bingwa wa dunia wa kuhifadhi mazingira inayotolewa kila mwaka na Umoja wa Mataifa. Tuzo hiyo amekabidhiwa leo mjini New Delhi, India ambako Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres yuko ziarani. 

Tumbaku inaharibu mazingira kuliko ilivyofahamika- Ripoti

Suala la matumizi ya tumbaku kuhatarisha afya ya binadamu limekuwa bayana miongo na miongo hata hivyo hii leo ripoti mpya imeweka dhahiri vile ambavyo tumbaku inasabaratisha mazingira.

Kilimo chaleta nuru kwa wakazi kaunti ya Meru, Kenya

Kilimo ndio uti wa mgongo ni usemi wenye maana kubwa sio tu kwa uchumi wa mataifa mengi yanayoendelea lakini pia kwa raia wa kawaida, na kwa mujibu wa shirikala Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo

Sauti -
4'37"

Usafi wa mazingira ni wajibu na jukumu la kila mtu-UNEP

Usafi wa mazingira ni muhimu sana na ni wajibu wa kila mtu, limesema leo shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na maendeleo UNEP.

Makazi mapya yanayozingatia mazingira yaleta ahueni kwa wakimbizi wa Yemen

Yemen, nchi iliyogubikwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe zaidi ya miaka mitatu sasa. Mamia ya maelfu ya raia wamefurushwa makwao na sasa wanaishi ndani au nje ya nchi hiyo. Maisha ya ukimbizini ni magumu na yanakuwa magumu zaidi pale ambapo makazi ambayo unaishi hayahimili joto wala baridi.

Sauti -
3'49"

Pamoja na habari njema, hatua zaidi zahitajika kuinusuru dunia:UNEP

Utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu au SDG’s unaipeleka dunia katika mwelekeo unaopaswa lakini bado juhudi zaidi zinahitajika kuhakikisha malengo hayo yanatimia hususan yanayohusiana na mazingira na mabadiliko ya tabianchi. 

Tusipotunza mazingira, hayatatutunza- Maloba

Utunzaji wa mazingira ni suala ambalo linahitaji ushiriki wa kila mtu kwani 'tusipotunza mazingira, hayatatutunza.' Hayo yamesemwa na Innocent Maloba kutoka shirika la World Wide Fund kwa ajili ya mazingira linalofanya kazi katika takriban nchi mia moja kote duniani. 

Sauti -
4'34"

Marufuku ya matumizi ya plastiki Uganda yasuasua

Idadi kubwa ya mifuko ya Plastiki inayotumika katika nchi nyingi duniani husususan nchi zinazoendelea ina madhara kwa ardhi, mito, baharí kutokana na kuwa haiozi.

Sauti -
4'

Twakata misitu twajiumiza wenyewe- Samia

Nchini Tanzania nako maadhimisho ya siku ya mazingira duniani yamefanyika kitaifa jijini Dar es salaam ambako Umoja wa Mataifa, serikali na wadau wameazimia kuendelea kushirikiana ili kudhibiti uharibifu wa mazingira.

Kisichofaa kutumika tena na tena achana nacho :Guterres

Kataa matumizi ya plastiki zinazotumika mara moja na kutupwa, ni kauli ya Umoja wa Mataifa katika siku ya maadhimisho ya siku ya mazingira duniani.