Mazingira

Twakata misitu twajiumiza wenyewe- Samia

Nchini Tanzania nako maadhimisho ya siku ya mazingira duniani yamefanyika kitaifa jijini Dar es salaam ambako Umoja wa Mataifa, serikali na wadau wameazimia kuendelea kushirikiana ili kudhibiti uharibifu wa mazingira.

Kisichofaa kutumika tena na tena achana nacho :Guterres

Kataa matumizi ya plastiki zinazotumika mara moja na kutupwa, ni kauli ya Umoja wa Mataifa katika siku ya maadhimisho ya siku ya mazingira duniani.

Plastiki ni fursa ya kipato kwa kijana Tanzania

Katika juhudi za kuhakikisha uhifadhi wa mazingira  serikali, kampuni na hata watu binafsi wanachukua hatua katika kurekebisha makosa ambayo yanasababisha uharibifu wa mazingira. Uwepo wa plastiki zinazotupwa kiholela ni moja ya kero kubwa lakini pia athari zake kwa mazingira ni mbaya kwani husababisha changamoto nyingi ikiwemo mafuriko. Katika kuelekea siku ya mazingira duniani kesho Juni 5, tunaelekea nchini Tanzania ambako Tumaini Anatory wa radio washirika Karagwe FM mkoani Kagera anaangazia kijana ambaye amegeuza taka hizo kuwa kiini cha kipato chake.

Sauti -
3'42"

Juhudi dhidi ya matumizi ya plastiki zitumikazo mara moja zapamba moto

Ulimwengu unahitaji ufumbuzi mbadala dhidi ya  matumizi ya vifaa vya plastiki vinavyotumika mara moja na kutupwa.