Mashujaa Halisi

Furaha yetu ni kupata majawabu Lamu bila urasimu - Umra

Katika maeneo ya ndani zaidi ya kaunti ya Lamu, kaskazini mashariki mwa pwani ya Kenya, huduma za afya zinakumbwa na changamoto kubwa.

Sauti -
1'42"

19 Agosti 2020

Jaridani la Umoja wa Mataifa hii leo na Flora Nducha

-Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibindamu na masula ya dharura OCHA yatoa shukrani zake kwa wahudumu wa kibinadamu kokote waliko katika kuokoa maisha.

Sauti -
13'27"

Furaha yetu ni kupata majawabu Lamu bila urasimu - Umra

Katika maeneo ya ndani zaidi ya kaunti ya Lamu, kaskazini mashariki mwa pwani ya Kenya, huduma za afya zinakumbwa na changamoto kubwa. Ni kwa mantiki hiyo kila mwezi madaktari na wafanyakazi wa shirika la kiraia la Safari Doctors hufunga safari kwa boti, wakiwa na shehena za dawa kwa ajili ya kutibu siyo tu binadamu bali pia wanyama. Safari  Doctors imeasisiwa na Umra Omar ambaye pia ndiye Mkurugenzi na pia miongoni mwa mashujaa halisi wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa kwa mwaka huu wa 2020.