Watu 95 wauawa nchini Mali, MINUSMA yalaani vikali
Mashambulizi dhidi ya raia wasio na hatia Mali ni ukatili usiostahili na unaopaswa kushughulikiwa haraka, umesema leo mpango wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu nchini humo MINUSMA baada ya shambulio la jana jioni kukatili maisha ya raia wengi kwenye Kijiji cha Sobanou-Kou kilichopo Kaskazini Mashariki mwa mji wa Bandiagara, kwenye jimbo la Mopti.