Mark Lowcock

CERF yatoa dola milioni 15 ili kusaidia manusura wa tetemeko Indonesia

Umoja wa Mataifa umetoa dola milioni 15 kutoka mfuko wake wa msaada wa dharura kwa ajili ya kusaidia manusura wa tetemeko la ardhi na tsunami vilivyokumba eneo la Sulawesi nchini Indonesia tarehe 28 mwezi uliopita wa Septemba.

Shambulio lingine lalenga watoto Yemen, OCHA yapaza sauti

Kwa mara nyingine tena ndani ya wiki mbili watoto nchini Yemen wameshambuliwa na kuuawa huko jimboni Hudaydah.

Watoto wengi nchini Syria wameteseka sana

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu watoto walio kwenye mizozo, Virginia Gamba, amesema zaidi ya watoto 7,000 wamepoteza maisha yao au wamejeruhiwa na kuachwa na ulemavu wa kudumu kutokana na mgogoro unaoendelea nchini Syria amesema hayo Ijumaa akihutubia Baraza la Usalama

Sauti -
1'27"

Nchini Syria watoto hawajui maana ya amani- UN

Zaidi ya watoto 7,000 wamepoteza maisha yao au wamejeruhiwa na kuachwa na ulemavu wa kudumu kutokana na mgogoro unaoendelea nchini Syria.

Msaada wa UN unaokoa maisha ya maelfu DPRK: Lowcock

Baada ya kutembelea miradi mbalimbali inayosaidiwa na Umoja wa Mataifa jimboni Hwanghae Jamhuri ya watu wa Korea au DPRK, msaidizi wa Katibu Mkuu kwa ajili ya masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura, amesema msaada huo unabadili maisha ya maelfu ya watu.

Hali ya kibinadamu si shwari Yemen : OCHA

Hali ya kibinadamu nchini Yemen inazidi kuzorota kutokana  kuongezeka kwa migogoro, vikwazo dhidi ya misaada ya kibinadamu na kupungua kwa uingizaji wa biashara muhimu hivyo kusababishwa mamilioni ya waYemen kukabiliwa  uhaba mkubwa wa chakula.

Hali niliyoikuta Sudan Kusini ni mbaya sana:Lowcock

Mkuu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Mark Lowcock leo anahitimisha ziara nchini Sudan Kusini. Amesema alichokishuhudia huko kinatisha na kusikitisha, jitihada zaidi zinahitajika ili kuleta suluhu ya kisiana ya amani ya kudumu.

Sauti -
2'3"

Nilichokishuhudia Sudan Kusini kinasikitisha:Lowcock

Nilichokishuhudia Sudan Kusini kwa maelfu ya watu waliotawanywa kinasikitisha, amesema msaidizi wa Katibu Mkuu wa masuala ya kibinadamu Mark Lowcock ambaye leo anahitimisha ziara ya siku mbili nchini humo.

Ukarimu wa wahisani waleta nuru kwa wasyria

Huko Brussels, Ubelgiji hii leo wahisani wamechangia jumla ya dola bilioni 4.4 kwa ajili ya wakimbizi wa Syria na ukanda wa Mashariki ya Kati.

Sauti -
1'39"

Dola bilioni 4.4 si haba kwa wasyria

Baada ya mashauriano na mazungumzo na pia kusikia kauli kutoka kwa wawakilishi wa wananchi wa Syria, wahisani wamefungua pochi zao na kuchangisha fedha kukuwamua wananchi hao ambao mustakhabali wao uko mashakani.