Mark Lowcock

Dhamira ipo katika kutekeleza makubaliano ya Stockholm, Yemen-Griffiths

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Yemen, Martin Griffiths leo amehutubia kikao cha Baraza la Usalama kwa njia ya video kuhusu kile alitaja kama hatua chanya katika utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa mjini Stockholm nchini Sweden.

Shehena ya chakula cha msaada Yemen iko hatarini kuoza- UN

Umoja wa Mataifa umesema suala la la kuyafikia maghala ya shirika la mpango wa chakula duniani, WFP, yaliyohifadhi shehena ya nafaka huko Hudaidah nchini Yemen linazidi kupata umuhimu zaidi kila uchao.

Makubaliano ya Stockholm yameleta matokeo chanya kwa kiasi fulani Yemen- Griffiths

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Yemen, Martin Griffiths ameliambia Baraza la Usalama la Umoja huo leo kuwa pande kinzani kwenye mzozo wa Yemen kwa kiasi kikubwa zimezingatia usitishwaji wa mapigano Hudaydah kwa mujibu wa makubalianao yaliyofikiwa mjini Stockholm, Sweden mwaka jana.

Tusibweteke na kilichotokea Sweden, hali bado ni tete Yemen- Lowcock

Matumaini kuhusu mustakabali wa Yemen kufuatia matokeo ya mkutano kati ya pande kinzani huko Sweden, yasisababishe tubweteke kwa kuwa bado hayajawa na athari ya moja kwa moja kwa wananchi wa kawaida.

Hali ya kupungua kwa mapigano Hudaida itunzwe.

Viongozi wa mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa wameonesha kufurahishwa na kupungua kwa mapigano katika mji wa Hudaida lakini pia wakaitumia nafasi hiyo kutoa wito kwa makundi yote yanayohusika.

Hali ya Yemen haiko katika hatihati ya kuwa zahma , tayari ni zahma kubwa:UN

Yemen inahitaji kupigwa jeki kiuchumi, usitishaji mapigano na  mshikamano wa kimataifa  mbali ya msaada wa kibinadamu endapo jumuiya ya kimataifa inataka kuepuka baa la njaa na kuwa majaji wa kuamua mtoto yupi aewe chakula na yupi akose au yupi anastahili kuishi na yupi kufa, wamesema leo viongozi wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa wakihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani.

 

Wakati wa kuchukua hatua Yemeni ni sasa: Guterres

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo akiwa katika katika makao makuu ya Umoja huo mjini New York Marekani, amesema kinachoendelea nchini Yemeni siyo janga la asili bali ni janga linalosababishwa na binadamu.

Baa la njaa lanyemelea Yemen- OCHA

Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu misaada ya kibinadamu, OCHA, Mark Lowcock amesema baa la njaa linanyemelea Yemen, nchi ambayo hivi sasa takribani nusu ya watu wake hawana chakula cha kutosha.

Misaada ya kibinadamu na maendeleo vinapaswa kwenda pamoja-UN

Mkuu wa shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP Achim Steiner na mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA, Mark Lowcock, hii leo Oktoba 7 wameikamilisha ziara yao ya kwanza ya pamoja nchini Chad.

Wadau wa kitaifa na kimataifa msisahau Nigeria-UN

Mkuu wa shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP Achim Steiner na mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA, Mark Lowcock, hii leo Oktoba 6 wakiwa Maiduguri, nchini Nigeria, wamewataka wadau wa kitaifa na kimataifa kuunganisha nguvu kushughulikia mahitaji muhimu ya kibinadamu katika maeneo yaliyoathiriwa na mgogoro katika majimbo ya kaskazini mashariki mwa Nigeria likiwamo jimbo la Borno, Adamawa na Yobe na pia kwa haraka kurejesha utaratibu wa maisha katika hali yake.