Kwa wananchi wa kawaida vitendo ni bora kuliko maneno au hotuba:Espinosa
Maneno matupu na hotuba bila vitendo halisi na hatua zinazoonekana katika kusongesha ajenda ya maendeleo endelevu, havina faida yoyote kwa mwananchi wa kawaida. Hayo yamesemwa leo na Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wakati wa ufunguzi wa hafla ya maadhimisho ya kwanza ya siku ya ushirikiano wa kimataifa na amani kwenye makao makuu ya Umoja huo mjini New york Marekani.