Mali

MINUSMA yakarabati bustani Timbuktu na sasa wakulima na wachuuzi wamenufaika

Nchini Mali, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu nchini humo, MINUSMA baada ya kuona athari za mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kwenye mbinu za kujipatia kipato miongoni mwa wakulima wa eneo la Timbuktu, uliibuka na mradi wa kuboresha bustani yao ya soko la mboga na sasa nuru ya kujipatia kipato imeonekana.
 

Utani baina ya makabila ni moja ya mbinu za kuchagiza amani na maelewano

Tofauti zinapaswa kuimarisha jamii badala ya kuisambaratisha, huo ndio  ujumbe uliotamalaki wakati wa kampeni iliyoendeshwa nchini Mali na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu nchini humo MINUSMA kwa kushirikiana na chama cha wadau wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MANU.

Sauti -
2'39"

23 Desemba 2021

Hii leo jaridani Assumpta Massoi anaanzia nchini Burundi ambako kijana mmoja baada ya kumaliza masomo ya elimu ya juu na kuona cheti chake hakimpatii ajira aliamua kuanzisha mradi wa kuku na sasa amekuwa chachu kwa jamii yake!

Sauti -
14'9"

Wajumbe wa Baraza la Usalama wawasili Mali kupata taswira halisi

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamewasili nchini Mali kwa ziara ya siku mbili, ikiwa ni sehemu ya ziara yao ya siku 5 kwenye ukanda wa Sahel, ziara ambayo pia  itawapeleka nchini Niger.
 

 Chondechonde vijana tuache itikadi kali, tukumbatie amani Sahel: Vieux Farka Touré.

 Mradi wa kuelimisha kuhusu ongezeko la machafuko , kutokuwepo usalama na watu kutawanywa kwenye eneo la Sahel umefanya kutungwa wimbo mahsusi na mtunzi kutoka Mali Vieux Farka Touré na kuimbwa na wanamuziki mbalimbali wa eneo hilo. 

Raia 50 wauawa Mali, Guterres asema ni ukiukwaji wa sheria za kimataifa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani vikali mashambulio yaliyofanywa dhidi ya raia tarehe 8 Agosti mwaka huu 2021 katika mkoa wa Gao nchini Mali ambapo raia takribani raia hamsini waliripotiwa kuuawa na kadhaa kujeruhiwa. 

Baraza la Usalama lalaani kitendo cha viongozi Mali kukamatwa

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamelaani vikali kitendo cha kukamatwa kwa Rais wa mpito wa Mali, Waziri Mkuu na maafisa wengine waandamizi wa serikali hiyo tarehe 24 mwezi huu wa Mei, kitendo kilichofanywa na maafisa wa jeshi la serikali ya Mali.

Walinda amani kutoka Uingereza walioko nchni Mali wapiga doria ya siku 28 Gao

Nchini Mali, kikosi maalum cha Uingereza kinachohudumu katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu nchini Mali, MINUSMA kimeendesha doria ya siku 28 kutoka mji wa Gao hadi Tassiga jimboni Gao kwa lengo la kulinda raia, katika eneo hilo ambalo limekuwa likishuhudia matukio ya ukosefu wa us

Sauti -
2'6"

Walinda amani wa Uingereza nchini Mali wapiga doria ya siku 28 Gao 

Nchini Mali, kikosi maalum cha Uingereza kinachohudumu katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu nchini Mali, MINUSMA kimeendesha doria ya siku 28 kutoka mji wa Gao hadi Tassiga jimboni Gao kwa lengo la kulinda raia, katika eneo hilo ambalo limekuwa likishuhudia matukio ya ukosefu wa usalama.

Walinda amani 4 wa UN wauawa Mali, 19 wajeruhiwa, Guterres azungumza

Walinda amani wanne wa Umoja wa Mataifa wanaohudumu nchini Mali wameuawa kwenye kambi yao huko Aquelhok jimboni Kidal, huku wengine 19 wamejeruhiwa, kitendo ambacho kimelaaniwa vikali na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Walinda amani hao ni raia wa Chad.