Katika ajenda ya maendeleo endelevu SDGs ya mwaka 2030, lengo namba 3 la afya bora kwa kila mtu, limekuwa changamoto kubwa sana hasa kwa nchi za Afrika zilizoko kusini mwa jangwa la sahara.
Bajeti ya umoja wa Mataifa kwa mwaka 2018-2019 yenye kurasa zaidi ya elfu 8 zilizosheheni maelezo ya mipango mbalimbali na takwimu za taasisi hii kubwa zaidi duniani ilipitishwa mwishoni mwa juma na nchi 193 wanachama wa Umoja huo ikiwa na upungufu wa mamilioni ya dola ikilinganishwa na mwaka 201
Nchini Papua New Guinea, wanawake wamechukua hatua kulinda afya zao. Baada ya safari za kutwa kucha kufuata vituo vya afya vilivyokuwa vinapatikana umbali mrefu, wanawake walishikamana na kusaka usaidizi kutoka Benki ya Dunia ili kuanzisha kituo cha afya kwenye kijiji chao.
Kwa zaidi ya miongo miwili sasa, Somalia imeghubikwa na migogoro ikiwemo mashambulizi ya Al-Shabaab na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, na hivyo kusababisha maelfu ya raia kupoteza maisha, makazi na wengine kusaka hifadhi nchi jirani.