Makala yetu wiki hii ambayo pia ni ya mwisho kwa mwaka huu wa 2012 inaangazia Azimio la aina yake lililopitishwa na Umoja wa Mataifa la kupiga vita ukeketaji wa wanawake.
Ulimwengu unaendelea kushuhudia dhuluma mbalimbali dhidi ya wanawake, ikiwemo ukatili, kwa madai eti ni utekelezaji wa mila na desturi za jamii husika.
Umoja mataifa kupitia msimamizi Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani, Herve Ladsous umetangaza bayana kuwepo kwa sintofahamu ya hali ya usalama huko Goma, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC.
Sauti yangu ina nafasi! Ni ujumbe wa siku ya kimataifa ya haki za binadamu iliyoadhimishwa tarehe 10 Desemba mwaka huu, siku ambayo miaka 64 iliyopita lilipitishwa tamko la kimataifa la haki za kibinadamu.
Siko seli au seli mundu ni miongoni mwa magonjwa yanayoendelea kutikisa nchi mbali mbali duniani ambapo kila mwaka watoto Laki Tatu huzaliwa na ugonjwa huo wa kurithi, na hizo ni takwimu za Shirika la afya duniani,