Makala za wiki

Mazungumzo kuhusu Mkataba wa Kimataifa juu ya Haki za Mtoto (Sehemu ya Pili)

Kwenye makala ya awali, ya mfululizo wa vipindi vya sehemu mbili kuhusu Mkataba wa Haki za Mtoto, makala iliotangazwa hapo jana, tulikupatieni mahojiano baina ya mwanafunzi wa kidato cha pili, kutoka Kenya, Millicent Atieno Odondo,

Mazungumzo kuhusu Mkataba wa Kimataifa juu ya Haki za Mtoto (Sehemu ya Awali)

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) majuzi lilichapisha ripoti muhimu yenye mada isemayo "Hali ya Watoto Duniani kwa 2009".

Mazungumzo ya Redio ya UM na mshindi wa mashindano ya picha ya UNDP/Olympus/AFP kutoka Kenya

Ijumatano raia wawili wa kutoka Kenya, pamoja na mzalendo mwanamke kutoka Morocco, walitunukiwa zawadi maalumu, kwa picha zao zilizoonyesha namna watu wa kawaida barani Afrika, wanavyoshiriki kwenye harakati za kutunza na kuhifadhi mazingira - ikijumlisha zile shughuli za kupandisha miti, na huduma za kuigeuza mifuko ya plastiki, iliotupwa kwenye majaa baada ya kutumiwa, kuwa mikoba ya pochi na vikapu, ikiwa miongoni mwa kadhia muhimu zinazochangia kimataifa katika kupunguza athari haribifu za mabadiliko ya hali ya hewa.

Suluhu hakika yahitajika kudhibiti upungufu wa maji unaosababishwa na hali ya hewa ya kigeugeu

Wiki hii tunajadilia umuhimu wa kuzingatia, kwa kina, mchango wa maji safi na salama, katika udhibiti bora wa mabadiliko ya hali ya hewa.

UM inahamisha na kuwatawanya wafanyakazi wake Afghanistan kuwapatia usalama unaoridhisha

Shirika la UM la Kuisaidia Afghanistan Kurudisha Utulivu (UNAMA) Alkhamisi lilitangaza ya kuwa limeamua kuhamisha baadhi ya wafanyakazi wake, waliopo katika sehemu kadha wa kadha nchini Afghanistan, na kuwapeleka kwenye makazi ya muda ndani ya nchi, na wengine nje ya taifa hilo, kwa matarajio ya kuwapatia ulinzi unaofaa.