Makala za wiki

Mataifa wanachama 187 yalaumu vikwazo vya Marekani dhidi ya Cuba kwenye Baraza Kuu

Mnamo Ijumatano ya wiki hii, kwa mwaka wa 18 mfululizo, wawakilishi wa kimataifa kwenye Baraza Kuu la UM walipiga kura ya kuunga mkono, kwa mara nyengine tena, azimio la kuishtumu Marekani kwa vikwazo vyake vya kiuchumi, kifedha na kibiashara dhdi ya Cuba.

Ofisa Mkuu Mtendaji wa Taasisi ya NEPAD azungumzia mwelekeo unaohitajika kusukuma mbele maendeleo Afrika

Mapema wiki hii, kabla ya kuzungumzia kikao cha Baraza Kuu la UM, kusailia ripoti kadha za KM, na kutoka wajumbe wa kimataifa na mashirika ya UM zilizozingatia huduma za kukuza maendeleo katika Afrika, Dktr Ibrahim Assane Mayaki, Ofisa Mkuu Mtendaji wa Taasisi ya Ushirikiano Mpya wa Maendeleo kwa Afrika (NEPAD), alifanya mahojiano maalumu na waandishi habari waliopo Makao Makuu.

Ripoti ya Goldstone inazingatiwa kwenye mjadala wa kila mwezi wa Baraza la Usalama juu ya Mashariki ya Kati

Ijumatano Baraza la Usalama liliitisha kikao, ambacho rasmi, kilidaiwa kuzingatia hali ya Mashariki ya Kati, kwa ujumla, kama inavyofanyika mara kwa mara, takriban kila mwezi, hapa kwenye Makao Makuu.

Ripoti ya mwaka ya UNICEF juu ya hifadhi ya watoto imesisitiza bidii zaidi zahitajika kuwalinda watoto dhidi ya udhalilishaji

Ripoti ya mwaka ya UNICEF kuhusu hifadhi ya watoto kimataifa imeeleza kwamba licha ya kuwa karibuni kulipatikana maendeleo kwenye suala hilo, watoto bado wanaendelea kudhalilishwa na kukabiliwa na vitendo karaha kadha wa kadha dhidi yao.

Mwanaharakati wa kuhifadhi mazingira ahimiza viongozi wa dunia kuharakisha mapatano ya kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa

Ripoti ya wiki hii itazingatia fafanuzi za mwanaharakati mashuhuri wa Afrika Mashariki anayetetea hifadhi ya mazingira ulimwenguni, kwa madhumuni ya kunusuru maisha ya vizazi vya siku za baadaye. Mwanaharakati huyo ni Profesa Wangari Maathai, mzalendo wa Kenya.