Makala za wiki

Ofisa wa UNHCR anasailia mzozo wa makazi kwenye kambi za wahamiaji za Dadaab, Kenya

Katika miezi ya karibuni, vurugu na mizozo ya kihali ilikithiri kwa wingi katika Usomali, hali iliosababaisha maelfu ya raia kuamua kuhama makwao na kuelekea mataifa jirani kutafuta hifadhi na usalama.

Mhudumia misaada ya kiutu wa kimataifa awapatia sauti wanusurika wa madhila ya kijinsiya katika JKK

Ijumatano ya tarehe 19 Agosti (2009) iliadhimishwa na UM, kwa mara ya kwanza katika historia yake, kuwa ni ‘Siku ya Kumbukumbu kwa Wahudumia Misaada ya Kiutu Duniani.\'

Waathirika wa chuki za wageni Afrika Kusini wanasema 'bora usalama badala ya anasa za maisha'

Taarifa ya Ofisi ya UM juu ya Huduma za Dharura (OCHA) iliotolewa wiki hii ilielezea mvutano uliozuka kwenye kambi ya makazi ya muda ya Bluewater, katika mji wa Cape Town ambapo wanaishi wahamiaji 396 ambao mnamo mwezi Mei 2008 walifukuzwa kwenye mastakimu ya muda kwa sababu ya tukio liliodaiwa kuwakilisha chuki za wazalendo dhidi ya wageni.

Vijana wa Kimataifa wakusanyika Geneva kuhudhuria mazoezi ya kitaaluma kwenye UM wa kuigiza

Mradi wa \'UM ya Majaribio\' ni aina ya mazoezi ya kitaaluma yanayoendelezwa kwenye maskuli na vyuo vikuu vya kimataifa takriban kila mwaka, katika sehemu kadha wa kadha za ulimwengu.

Wamaasai wa Kenya wanatazamiwa kuhifadhi mila za kijadi kwa msaada wa WIPO

Mnamo mwisho wa Julai, kwenye sherehe ya jumuiya, iliofanyika chini ya kivuli cha mti wa mkangazi, na kuhudhuriwa na wenyeji wa asili 200, Chifu Kisio na wazee wengine wa Jumuiya ya Wamaasai wa Il Ngwesi, Laikipia, Kenya walikabidhiwa rasmi vifaa vya mawasiliano ya kisasa, vya kurikodia na maofisa wa Shirika la UM juu Ya Hakimiliki za Taaluma Duniani (WIPO).