Makala za wiki

UNHCR inasailia majaaliwa ya wahamiaji wa Kisomali katika Kenya

Mapema wiki hii Shirika la UNHCR liliripoti wasiwasi wake kuhusu taarifa ilizopokea zilizothibitisha kwamba Serikali ya Kenya huwarejesha makwao kwa nguvu makwao,wale wahamiaji wa Kisomali wenye kuomba hifadhi ya kisiasa.

FAO imeanzisha taadhima rasmi za Mwaka wa Kimataifa juu ya Fumwele Asilia

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) wiki hii limeanzisha rasmi taadhima maalumu za Mwaka wa Kimataifa juu ya Ufumwele wa Asili.

Makao Makuu ya UM yafadhiliwa dokezi ya Tamasha ya FESMAN 2009

Maofisa wa UM Ijumatano walipata fursa ya kushuhudia kwenye Makao Makuu, dokezo ya shamrashamra zitakazokuwepo kwenye Tamasha Kuu ya 2009 kuhusu Utamaduni wa KiAfrika, zitakazofanyika kwenye mji wa Dakar, Senegal kuanzia tarehe 1 mpaka 21 Disemba 2009.

Mataifa Wanachama yajaribu kukomesha msiba uliopamba Ghaza

Wiki hii, Baraza la Usalama limefanyisha kikao, cha ngazi ya juu, cha siku mbili kuzingatia hali katika Tarafa ya Ghaza, kikao ambacho kilianza majadiliano Ijumanne usiku, Januari 06 na kuendelea hadi Ijumatano Januari 07 (2009), ambapo wajumbe wa Mataifa Wanachama 15 walishindwa kupitisha azimio la kusimamisha haraka mapigano katika eneo la Ghaza.~

BU na KM wasailia hali baada ya kuingia Ghaza kwa majeshi ya Israel

KM Ban Ki-moon, kwenye taarifa iliotolewa na msemaji wake, alinakiliwa akisema ameingiwa na “wasiwasi mkubbwa kuhusu athari mbaya kufuatia kuanzishwa kwa operesheni za ardhini za vikosi vya Israel katika Tarafa ya Ghaza” Ijumamosi (03/01/2009), wakati ambao Baraza la Usalama (BU) vile vile liliamua kuitisha kikao cha dharura kuzingatia hali hiyo ya uhasama Ghaza.

Kumbukumbu za majadiliano kuzingatia muongezeko wa vurugu katika Ghaza

Ifuatayo ni kumbukumbu ya kikao cha Baraza la Usalama, kilichofanyika Ijumatano kwenye Makao Makuu ya UM, kuanzia saa 12:40 magharibi hadi saa 2:45 usiku.~