Makala za wiki

KM azungumza na waandishi habari juu ya ziara yake ijayo katika Sudan, Chad na Libya

Ijumanne, Agosti 28 (2007) Katibu Mkuu (KM) wa Umoja wa Mataifa (UM) Ban Ki-moon alikuwa na mazungumzo na waandishi habari katika Makao Makuu juu ya ziara yake katika mataifa ya Chad, Libya na Sudan kusailia kipamoja na viongozi wa mataifa haya juu ya taratibu zitakazosaidia kurudisha utulivu na suluhu ya kuridhisha kuhusu tatizo la Darfur. KM alianza mazungumzo kwa kuelezea sababu hasa zilizomhamasisha yeye binafsi kuamua kufanya ziara hii:

Wanamazingira Vijana Wakusanyika Ujerumani Kujadilia Hifadhi Bora ya Mazingira Duniani

Kuanzia tarehe 26 hadi 30 Agosti 2007, katika mji wa Leverkusen, Ujerumani kulifanyika Mkutano wa Tatu wa Vijana wa Kimataifa wa Tunza, ulioandaliwa na Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira Duniani (UNEP).

Makundi ya wanamgambo 3,500 katika Ituri kukubali kusalimisha silaha

Makundi matatu ya wanamgambo wa JKK katika wilaya ya Ituri, yaani Mouvement Revolutionnaire Congolais (MRC), Front de Résistance Patriotique de l’Ituri (FRPI) na Front des Nationalistes et Intégraionnistes (FNI) yameahidi kusajili jumla ya wapiganaji wao 3,500 kwenye ule mpango wa UNDP ujulikanao kama mradi wa DDR, mpango ambao utawawezesha wanamgambo husika kupatiwa msaada wa fedha za kuanzisha maisha mapya ya kiraia au kujiunga na jeshi la taifa.

Mzozo wa mgomo wa watumishi wazalendo wa MONUC katika DRC

Jumuiya ya Watumishi Wazalendo walioajiriwa na Shirika la UM linalosimamia ulinzi wa amani katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, yaani Shirika la MONUC, Alkhamisi iliamua kuitisha mgomo baridi, uliosababishwa na madai ya kwamba wenye kusimamia utawala katika MONUC walipuuza kwa muda mrefu malalamiko yao ya kikazi na kushindwa kuwapatia suluihu ya kuridhisha. Tulifanya mahojiano ya simu na mwandishi habari aliopo mjini Kinshasa, DRC anayeitwa ‘Ahmed Simba’ ambaye alitupatia dokezo kuhusu mgomo huu. Alianza kwa kuelezea nini hasa kilikuwa chanzo cha mgomo.~~Sikiliza mahojiano kamili kwenye idhaa ya mtandao.

Juhudi za kuisaidia Uganda kukabiliana na mafuriko.

Ofisi ya UM inayohusika na Misaada ya Dharura, au Ofisi ya OCHA, imeripoti kwamba eneo la Uganda mashariki limekabwa na mafuriko makubwa baada ya mvua kali kunyesha katika mwisho wa Julai.

Kuongezeka kwa ghasia dhidi ya vyombo vya habari huko Somalia

Kwa mara nyingine vyombo vya habari huru huko Somalia vyapoteza waandishi habari wawili mwishoni mwa wiki iliyopita. Ali Iman Sharmarke muanzilishi na mwenyekiti wa kituo mashuhuru cha redio na televisheni pamoja na mwandishi habari wa kipindi mashuhuri Mahad Ahmed Elmi wa kituo hicho hicho, waliuliwa karibu wakati mmoja huko Mogadishu.

Siku ya Kimataifa ya Wazawa

Karibu wazawa milioni 370 kote duniani wanaendelea kubaguliwa, kutengwa na kuishi katika hali ya umaskini kabisa na ghasia, Katibu Mkuu wa UM bw Ban Ki-moon, alitoa mwito wa kuchukuliwa hatua za dharura kukabiliana na matatizo hayo.

Ajali ya treni huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Tukiendelea na makala ya Jarida wiki hii, kama mlivyo sikia kwenye taarifa ya habari kulitokea ajali mbaya ya treni huko karibu na mji wa Kakenge, jimbo la Kasai ya Magharibi DRC.

Mkutano wa viongozi juu ya kuimarisha taasisi na ujuzi wa Waafrika katika Maendeleo

Mkutano wa pili wa viongozi juu ya kuimarisha uwezo wa utekelezaji wa nchi za Kiafrika ulimalizika mjini Maputo hii leo.