Makala za wiki

Siku ya Kufyeka Malaria Afrika

Wiki hii, Jumuiya ya Ushirikiano wa Kurudisha Nyuma Malaria imewasilisha mradi mpya wa kufadhilia huduma za kupiga vita maradhi ya malaria Afrika. Jumuiya hiyo inatumai kwamba nusu ya maombi yote ya yale mataifa yanayohitajia msaada huo yatatekelezewa mataifa husika, hususan katika bara la Afrika, eneo ambalo, kila mwaka, asilimia 90 ya vifo milioni 1 vya malaria hutukia.

Vurugu la Usomali limefurutu ada, na ni la hatari mno

Ijumanne, Makamu KM juu ya Misaada ya Dharura, John Holmes aliripoti mbele ya Baraza la Usalama kwamba hali ya mapigano nchini Usomali kwa sasa ni mbaya sana, hususan kwenye mji wa Mogadishu. Holmes aliirudia tena taarifa hii pale alipokutana na waandishi habari wa kimataifa waliopo Makao Makuu:~

Balozi wa Kenya azingatia mkataba mpya dhidi ya silaha ndogo ndogo

Mwakilishi wa Kudumu wa Kenya katika UM, Balozi Zachary Muburi-Muita alifanya mahojiano na Redio ya UM ambapo alizungumzia, na kuzingatia yale mapendekezo ya baadhi ya wanadiplomasiya wa kimataifa - akiwemo pia Kamishna Mkuu Mstaafu wa Haki za Binadamu, Mary Robinson - ya kuanzisha kampeni ya kubuni chombo kipya cha sheria ya kimataifa ili kudhibiti bora biashara ya silaha ndogo ndogo ulimwenguni.

Sudan imekubali furushi la ulinzi wa amani kwa Darfur

Serekali ya Sudan wiki hii ilituma barua kwa Baraza la Usalama ilioelezea kukubali kupelekwa katika Darfur helikopta zitakazotumiwa na vikosi vya mseto vya AU na UM katika shughuli za kuimarisha usalama na amani kwa raia wa jimbo la magharibi la Sudan la Darfur.

Baraza la Usalama kuzingatia, kwa mara ya kwanza, athari za mabadiliko ya hali ya hewa duniani

Wataalamu wa kimataifa katika fani ya sayansi wanaashiria ya kuwa mali ya asili ya maji, pamoja na ardhi, zitaendelea kuadimika polepole katika siku zijazo. Kadhalika inakhofiwa mabadiliko ya hali ya hewa, hali kadhalika, kama hayajadhibitiwa mapema, huenda yakazusha maangamizi yasiorudishika na kugeuza milele sura ya sayari yetu.

UM unakumbuka mauaji ya Rwanda

Tarehe 09 Aprili, iliadhimishwa na UM kuwa ni siku ya kuukumbuka umma wa Rwanda ulioteswa na kuuliwa kikatili miaka 13 iliopita. Kwa mujibu wa ripoti za kimataifa, makundi ya majambazi na maharamia, waliokuwa wamechukua mapanga na mabunduki, waliamua kumaliza mauaji yao ya kikatili yalioangamiza watu 800,000 ziada kutoka sehemu zote za Rwanda.

Juhudi za UM kudhibiti maradhi ya vijidudu vinavyodhuru ngano

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limeripoti kugundua aina ya vijidudu vijiyoga vipya, vyenye uwezo wa kuzusha maambukizo haribifu makubwa ya mazao ya ngano, vijidudu ambavyo vimeshuhudiwa kusambaa kwenye maeneo yalioanzia Afrika Mashariki - ikijumuisha mataifa ya Ethiopia, Kenya na Uganda – na kuenea hadi Yemen, kwenye Ghuba ya Bara Arabu.

Fafanuzi juu ya Mkataba mpya wa Kuhifadhi Haki na Utu wa Watu Walemavu Duniani

Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Watu Walemavu Zanzibar (UWZ), Maalim Khalfan Hemed Khalfan, anayewakilisha pia shirika lisio la kiserekali la kimataifa linaloitwa Disabled Persons International (DPI) alikuwa miongoni mwa wajumbe kadha wa kimataifa, waliohudhuria katika wiki iliopita taadhima zilizofanyika kwenye ukumbi wa Baraza la Kuu la UM, New York, ambapo wawakilishi wa nchi wanachama 80 ziada walikusanyika kutia sahihi Mkataba mpya wa Kuhifadhi Haki na Utu wa Watu Walemavu Duniani. Idadi hiyo ilikiuka rikodi ya kihistoria kuhusu jumla ya ya nchi zilizotia sahihi mkataba mpya wa kimataifa, kwa mara ya kwanza.~~

Maendeleo ya uchumi Afrika yameegamia msingi dhaifu: ECA

Mnamo mwanzo wa wiki, Ejeviome Eloho Otobo, ofisa mchumi wa UM, aliyewahi kufanya kazi na Kamisheni ya UM juu ya Maendeleo ya Uchumi kwa Afrika (ECA), iliopo Addis Ababa, Ethiopia aliwakilisha mbele ya waandishi habari wa kimataifa kwenye Makao Makuu ripoti yenye muktadha usemao \'Taarifa juu ya Hali ya Uchumi Afrika 2007\'. Alisema uchumi wa Afrika, kwa ujumla, uliendelea kukuwa kwa asilimia tano mnamo miaka mitatu iliopita, lakini mwelekeo huo uliselelea kwenye msingi dhaifu sana.~