Makala za wiki

UM waashiria mwelekeo wa uchumi wa dunia kwa 2007

Katika kila mwanzo wa mwaka, UM huwasilisha ripoti maalumu kuhusu mwelekeo wa maendeleo ya uchumi duniani, ripoti ambayo huandaliwa na idara mbalimbali za UM, ikijumuisha Idara Inayohusika na Masuala ya Kiuchumi na Jamii (DESA), Shirika la UM kuhusu Maendeleo ya Uchumi na Biashara (UNCTAD) pamoja na kamisheni tano za kikanda zinazoshughulikia huduma za uchumi, yaani Kamisheni ya ECA, kwa Afrika, ECE, kwa Mataifa ya Ulaya, ECLAC, kwa Amerika ya Latina na Maeneo ya Karibiani, ESCAP, kwa mataifa ya Asia na Pasifiki na vile vile Kamisheni ya ESCWA, inayohusika na maendeleo ya Asia ya Magharibi. ~~

Katibu Mkuu Ban Ki-moon ameanza kazi na kuteua maofisa wapya wa ngazi za juu, akiwemo Naibu KM

Januari 01, 2007 Ban Ki-moon, aliyekuwa Waziri wa Masuala ya Nchi za Kigeni wa Jamhuri ya Korea au Korea ya Kusini, alianza kazi rasmi kama ni KM wa nane wa Umoja wa Mataifa.

Juhudi za UM kusuluhisha matatizo ya Pembe ya Afrika

KM Ban Ki-moon ametangaza taarifa maalumu iliyoyahimiza makundi yanayohasimiana Usomali kushirikiana na jumuiya ya kimataifa kukomesha, halan, vitendo vyote vya umwagaji damu.”