Makala za wiki

Mzozo wa Darfur unavyosababisha matatizo ya usalama kwa majirani wa Sudan.

Wakati majadiliano yanaendelea kwenye baraza la usalama katika kumaliza kuandika azimio litakalo ruhusu kupelekwa kwa kikosi cha pamoja cha Umoja wa Mataifa na Jumuia ya afrika huko Darfur, mzozo huo katika eneo la magharibi ya Sudan umekua na athari kubwa kwa majirani zake Chad na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Tatizo la uhamiaji

TY:Tukiendelea na makala ya Jarida wiki hii, tunazungumzia tatizo la uhamiaji, ambalo limekua likijadiliwa sana mwezi huu hasa wakati wa mkutano wa kimataifa juu ya uhamiaji na maendeleo mjini Brussels, Ubelgiji.

Siku ya idadi ya watu

Dunia nzima iliadhimisha siku ya kimataifa ya idadi ya watu chini ya mada “wanaume kama washirika wa afya ya uzazi”. Sherehe mbali mbali zilifanyika kote duniani na abdushakur ana ripoti kamili.

Wapiganaji wa Ituri DRC warudisha silaha zao

Awamu ya tatu ya zowezi la kuwapokonywa silaha wapiganaji wa zamani wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo huko jimbo la Ituri ilianza wiki hii.

Ushirikiano wa Jumuia ya Afrika na Umoja wa Mataifa wasifiwa na Naibu katibu mkuu

Naibu katibu mkuu wa UM, Bi Asha-Rose Migiro yuko ziarani baraani afrika na miongoni mwa mambo muhimu wakati wa ziara yake alihutubia ufunguzi wa mkutano wa viongozi wa Jumuia ya afrika AU huko Accra Ghana, pamoja na kufungua mkutano wa kimataifa juu ya wanawake huko Nairobi nchini Kenya.

Umoja wa Mataifa waomba msaada kupambana na utapia mloo

Na ripoti yetu ya pili kwa hii leo ni kwamba mashirika ya Umoja wa Mataifa huko Kenya yalitangaza wiki hii kwamba wanahitaji dola milioni 32 kutoka kwa wafadhili ili kuweza kupunguza kiwango cha utapia mloo ambacho wamesema kimefikia hali ya hatari miongoni mwa watoto chini ya miaka mitano ndani ya makambi ya wakimbizi. ~