Vijana hutumia mbinu mbalimbali ili kukidhi mahitaji ya maisha yao ya kila siku na fani ya ulimbwende au uanamitindo imekuwa ni moja ya fani zinazowavutia vijana , kwanza ikiwajengea umaarufu mkubwa lakini pia kuwasaidia kuwa na ajira ya kikidhi mahitaji yao.
Umoja wa Mataifa unaendelea kupigia chepuo usambazaji wa huduma za kujikinga na virusi vya ukimwi, VVU ikiwa ni moja ya utekelezaji wa lengo namba 3 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.
Ama kweli wahenga walinena kuwa mchumia juani, hulia kivulini na methali hiyo imedhihirika kwa raia mmoja wa Nigeria ambaye baada ya kupitia machungu mengi kwenye mikono ya wasafirishaji haramu, sasa ametulia tuli.