Makala za wiki

Burundi imepiga hatua kubwa katika kuboresha afya ya uzazi

Ni miaka isiyozidi mitano iliyosalia kabla ya 2015 muda ambao ni kikomo cha utekelezaji wa malengo yote manane ya maendeleo ya milenia yaliyoafikiwa na viongozi wa dunia mwaka 2000. Burundi ikiwa ni mmoja wa wao

Mahaka ya ICC yawaambia vigogo sita wa Kenya sheria ni msumeno

Mwendesha mashitaka mkuu wa ICC bwana Luis Moreno Ocampo mapema wiki hii aliamua kumaliza ngojangoja waliyokuwa nayo mamilioni ya Wakenya kutaka kujua ni nani hasa walikuwa vinara wa kuchochea ghasia zilizozuka baada ya uchaguzi mkuu wa Rais Desemba 2007 na mwanzoni mwa 2008 nchini humo.

Lengo la milenia la kutokomeza maradhi bado ni changamoto nchini Tanzania

Ikiwa imesalia miaka 5 tuu kabla ya kufikia 2015 muda wa mwisho uliafikiwa na viongozi wa dunia kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia, kila nchi hivi sasa inajitahidi japo kufikia nusu ya malengo hayo.

Bila kuwakwamua walemavu hatuwezi kutokomeza umasikini:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amezitolea wito serikali zote kuongeza juhudi kuwasaidia walemavu kwani amesema bila kutatua matatizo yao , vita dhidi ya umasikini, maradhi na maendeleo duni hatuwezi kuvishinda.

Hatua iliyopigwa Kenya kutimiza lengo la milenia la usawa wa kijinsia

Tatizo la kutokuwepo kwa usawa wa kijinsia katika nchi nyingi zinazoendelea bado ni kubwa.

Siku ya kimataifa ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake

Kila mwaka tarehe 25 Novemba ni siku ya kimataifa ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake na wito umetolewa kwa serikali, jumuiya za kijamii, mashirika yasiyo ya kiserikali na wadau wote wanaopigania haki za wanawake kuhakikisha udhalimu huo unamalizwa.

Tutasalia Somalia fedha na vifaa vikipatikana:Jeshi la Burundi

Serikali ya Burundi imesema vikosi vyake vya kulinda amani vilivyojumuishwa kwenye vikosi vya muungano wa Afrika AMISOM nchini Somalia visalia endapo tuu msaada na mahitaji muhimu yakipatikana.

Tukishirikiana bega kwa bega tutafikia malengo ya milenia Tanzania:Pinda

Viongozi wa nchi 20 zilizoendelea kiuchuni duniani yaani G-20 wamehitimisha mkutano wa Ijumaa hii mjini seoul Korea.

Hatua imepigwa katika kuleta amani maziwa makuu:Mulamula

kongamano la kimataifa la amani ya kanda ya maziwa makuu limesema lina matumaini ya amani zaidi.

Wanawake wanaendelea kuwa na jukumu muhimu katika ulinzi wa amani

Umoja wa Mataifa umesema utaendelea kuwa msitari wa mbele ili kuhakikisha wanawake wanashirikiwa ipasavyo katika masuala ya utafutaji wa amani na usalama na pia ngazi ya maamuzi.