Makala za wiki

Jan Pronk ataendelea kuwa Mwakilishi Maalumu wa UM kwa Sudan

Wiki hii KM Kofi Annan alikutana kwa mashauriano na Jan Pronk, Mjumbe wake maalumu anayeongoza lile Shirika la Ulinzi wa Amani la UM nchini Sudan, yaani UNMIS. Hivi majuzi Serekali ya Sudan iliripotiwa kumpiga marufuku Pronk kuwepo nchini.

Jukumu la wachoraji makatuni kustawisha amani duniani

Mapema wiki hii Idara ya Habari ya UM iliandaa semina maalumu iliyohudhuriwa na wachoraji makatuni mashuhuri wa kimataifa ambao walibadilishana mawazo juu ya taratibu zifaazo kutumiwa kwenye usanii wao zitakazosaidia kusukuma mbele amani na, hatimaye, kukomesha ile tabia ya kutovumiliana kati ya raia wa tamaduni tofauti. ~

Wahamiaji wa Burundi katika Tanzania kupatiwa makazi mapya Marekani

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti kuwa Serekali ya Marekani ipo tayari kuwapatia makazi mapya wale wahamiaji 13,000 wa Burundi pamoja na wazawa wao ambao wanayoyoma kwenye kambi za wahamiaji nchini Tanzania tangu 1972 pale walipokimbia mauaji ya halaiki nchini mwao.

Siku ya Kimataifa kupunguza Maafa

Ijumatano, tarehe 11 Oktoba iliadhimishwa kuwa ni ‘Siku ya Kimataifa Kupunguza Maafa’.

Ripoti kuhusu tatizo la utumiaji nguvu dhidi ya wanawake

Mapema wiki hii, KM Kofi Annan aliwasilisha mbele ya Kamati ya Tatu ya Baraza Kuu, ambayo inahusika na masuala ya kijamii, kiutu na kitamaduni, ripoti maalumu inayozingatia tatizo sugu, na karaha, la utumiaji nguvu dhidi ya wanawake.

KM kuanzisha rasmi mfuko wa ujenzi wa amani

Ijumatano KM Kofi Annan alishiriki kwenye kikao maalumu cha kuanzisha Mfuko wa Ujenzi wa Amani wa UM utakaotumiwa kuyasaidia yale mataifa yanayoibuka kutoka hali ya uhasama kurudisha amani kwenye maeneo yao na kujiepusha na hatari ya kuteleza tena kwenye mapigano, vurugu na machafuko.

UM unaadhimisha 'Siku ya Makazi Bora Duniani' kwa kuhimiza kuchukuliwe hatua za dharura kudhibiti ukuaji wa mitaa ya mabanda

Mapema wiki hii, kulifanyika sherehe kadha wa kadha katika miji mbalimbali ya dunia kuadhimisha ‘Siku ya Makazi Bora Duniani.’ Mada ya mwaka huu inasema: “Miji, ndiyo ni kivutio cha matarajio mema.”

Hali ya usalama katika Darfur yazidi kuharibika

Shirika la UM juu ya Huduma za Amani katika Sudan (UNMIS) limeripoti kuwa hali ya usalama katika Darfur ya kusini, inaendelea kuharibika, hususan katika mji wa Gereida, kutokana na mvutano uliojiri na uhasama kati ya makabila yanoishi kwenye eneo hilo. Wakati huo huo kwenye mji wa Um al-Kher, Darfur ya Magharibi imeripotiwa kutukia vifo vya watu walioambukizwa na maradhi ya kipindupindu. Ripoti ya karibuni ya KM imeonya ya kuwayale mashirika yanayohudumia misaada ya kiutu huenda yakafunga operesheni zake pindi hali ya usalama haijadhibitiwa katika eneo kama ipasavyo. ~~