Makala za wiki

Maelfu ya wahamiaji wa Usomali wakimbilia Kenya kunusuru maisha

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeripoti ya kuwa maelfu ya wahamiaji kutoka Usomali wanakimbilia Kenya hivi sasa kukwepa mapigano yaliofumka karibuni nchini mwao baina ya wafuasi wa Umoja wa Mahakama za Kiislamu (ICU) na vikosi vya Serekali ya Mpito.

UNICEF yawakilisha ripoti kuhusu maamirisho ya lengo la MDGs juu ya maji safi na usafi wa mastakimu

Mkurugenzi Mkuu wa UNICEF, Ann Veneman Alkhamisi aliwakilisha mbele ya waandishi habari wa kimataifa, ripoti yenye kuelezea maendeleo yaliopatikana kuhusu utekelezaji wa lengo la MDGs la kuimarisha huduma za maji safi na usafi wa mastakimu. Kwa mujibu wa ripoti ya UNICEF, tangu 1990 watu bilioni 1.2 walifanikiwa uwezo wa kupata maji ya kunywa safi na salama.

Mukhtasari unaongaza wiki ya kwanza ya mjadala wa wawakilishi wote katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa

Mjadala wa kila mwaka wa wawakilishi wote kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ulifunguliwa rasmi hapo Ijumanne, tarehe 19 Septemba (2006) na Sheikha Haya Rashed Al Khalifa wa Bahrain. Sheikha Haya katika hotuba yake ya ufunguzi aliwahimiza viongozi wa kimataifa waliokusanyika kwenye Makao Makuu kulenga zaidi juhudi zao katika kutekeleza kwa vitendo ahadi zao ili kusaidia kupunguza ufukara na kuboresha maisha ya umma wa kimataifa, kwa ujumla. ~

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limeitisha Mkutano wa Hadhi ya Juu kuzingatia misaada ya maendeleo kwa LDCs.

Mapema wiki hii kulifanyika kikao maalumu cha siku mbili katika Baraza Kuu kuzingatia juhudi za kupunguza umaskini na ufukara katika yale mataifa yenye uchumi mdogo kabisa, ambayo pia hujulikana kama mataifa ya LDCs. Wawakilishi wa kimataifa walikutana kwenye mjadala uliofanya mapitio ya ule Mpango wa Utendaji wa Brussels wa 2001.~~

Kumbukumbu ya ziara ya Makamu KM juu ya Masuala ya Kiutu katika Afrika

Mapema wiki hii Jan Egeland, Makamu KM Juu ya Misaada ya Kiutu ya Dharura alikutana na waandishi habari mjini Nairobi, Kenya baada ya kukhitimisha safari ya siku nane kwenye maeneo matatu yaliokabiliwa na matatizo ya kiutu barani Afrika; yaani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (JKK), Uganda na Sudan ya Kusini.

Mratibu wa Idara ya Huduma za Dharuru ya Umoja wa Mataifa ziarani Afrika

~Mratibu wa idara ya huduma za dharura ya Umoja wa Mataifa Bw. Jan Egeland akiwa ziarani huko Afrika ya kati alianza ziara yake huko Kongo mashariki, kwa kutemebelea kambi za wakimbizi na watu walioathirika sana na mapigano nchini humo.

Serikali ya Somalia kuanza mazungumzo ya amani mjini Khartoum

Wajumbe wa serekali ya mpito ya Somalia na wale wa Baraza la mahakama ya kiislamu linalodhibiti mji mkuu wa Mogadishu na sehemu kubwa ya nchi, wanaanza duru ya pili ya mazungumzo ya amani mjini Khartoum hii leo. Abdushakur Aboud amezungumza na mbunge na waziri mdogo wa zamani Hussein Bantu huko Baido na kumuliza kwanza mazungumzo yatahusu masuala gani. ~~

Wajumbe kutoka nchi mbali mbali duniani wakubaliana juu ya haki za walemavu

Baada ya miaka mitano ya majadiliano wajumbe kutoka karibu mataifa 100 ya dunia walikutana kwenye makao makuu ya umoja wa mataifa hapa New York, mwishoni mwa mwezi wa Agosti walikubaliana juu ya mkataba mpya wa kulinda haki za watu wenye ulemavu.