MAIDUGURI

Fanyeni kila muwezalo kutimiza ndoto zenu-Amina J. Mohammed

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed ambaye yuko ziarani Afrika Magharibi na ukanda wa Sahel amewachagiza wasichana katika eneo la Maiduguri jimbo la Borno nchini Nigeria kufanya kila wawezalo kutimiza ndoto zao kwani hakuna linaloshindikana. 

Sauti -
1'38"

Unaweza kuwa chochote utakacho la msingi imani na kujitume:Mohammed 

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed ambaye yuko ziarani Afrika Magharibi na ukanda wa Sahel amewachagiza wasichana katika eneo la Maiduguri jimbo la Borno nchini Nigeria kufanya kila wawezalo kutimiza ndoto zao kwani hakuna linaloshindikana. 

UN yalaani shambulio la karibuni zaidi nchini Nigeria

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani vikali shambulio la hivi karibuni zaidi lililofanywa jimboni Borno nchini Nigeria na kusababisha vifo vya raia.

Watoto waachiliwa huru Nigeria, UNICEF yajipanga kuwawezesha kumudu maisha ya uraiani

Watoto takriban 900 waliokuwa wakishikiliwa na makundi mbalimbali yenye silaha Kaskazini Mashariki mwa Nigeria wameachiliwa huru na makundi mbalimbali yenye silaha na kufanya idadi ya walioachiliwa na makundi hayo tangu mwaka 2017 kufikia zaidi ya 1700. Amina Hassan na taarifa zaidi.

Sauti -
2'1"

OCHA yatoa neno baada ya Jeshi la Nigeria kuwahamisha takribani watu 10,000 kutoka katika mji wao wa Jakana usiku wa manane

Mratibu wa wa shirika la Umoja wa Mataifa na kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura OCHA , Edward Kallon leo ametoa wito kwa serikali ya Nigeria kutoa msaada wa kibinadamu na kuwalinda watoto, wanawake na wanaume takribani 10,000 ambao walilazimishwa kuhamia katika mji mkuu wa jimbo la Borno, Maiduguri, wakitokea katika mji wao ulioko takribani kilomita 40 kutoka walikohamishiwa.

Dola milioni 848 zahitajika kunusuru wakimbizi wa ndani kaskazini-mashariki mwa Nigeria

Nchini Nigeria, Kuongezeka kwa mapigano kati ya vikosi vya serikali na makundi yaliyojihami kaskazini mashariki mwezi uliopita wa Desemba na kumesababisha watu wengi zaidi kufurushwa makwao kutoka eneo la Baga na kuelekea kwenye kambi za wakimbizi wa ndani hujo Maiduguri na Manguno ambako tayari

Sauti -
55"

Dola milioni 848 zahitajika kunusuru wakimbizi wa ndani kaskazini-mashariki mwa Nigeria

Nchini Nigeria, Kuongezeka kwa mapigano kati ya vikosi vya serikali na makundi yaliyojihami kaskazini mashariki mwezi uliopita wa Desemba na kumesababisha watu wengi zaidi kufurushwa makwao kutoka eneo la Baga na kuelekea kwenye kambi za wakimbizi wa ndani hujo Maiduguri na Manguno ambako tayari  kuna msongamano. John Kibego na taarifa zaidi.

Kundi la wapiganaji la CJTF lawaachia watoto 833 kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, limekaribisha kitendo cha kundi la wapiganaji la Civilian Joint Task Force (CJTF) mjini Maiduguri, kaskazini mashariki mwa Nigeria, kuwaachilia huru watoto 833 ikiwa ni sehemu ya ahadi yake ya kuacha kuwatumia watoto katika mapigano.

Wadau wa kitaifa na kimataifa msisahau Nigeria-UN

Mkuu wa shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP Achim Steiner na mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA, Mark Lowcock, hii leo Oktoba 6 wakiwa Maiduguri, nchini Nigeria, wamewataka wadau wa kitaifa na kimataifa kuunganisha nguvu kushughulikia mahitaji muhimu ya kibinadamu katika maeneo yaliyoathiriwa na mgogoro katika majimbo ya kaskazini mashariki mwa Nigeria likiwamo jimbo la Borno, Adamawa na Yobe na pia kwa haraka kurejesha utaratibu wa maisha katika hali yake.