Umoja wa Mataifa waadhimisha miaka 75 ya Nakba ya Wapalestina
Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Utekelezaji wa Haki Zisizozuilika za Watu wa Palestina, kwa usaidizi wa Idara ya Haki za Wapalestina, hii leo imedhimisha kumbukumbu ya miaka 75 ya Nakba katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Kwa mara ya kwanza katika historia ya Umoja wa Mataifa, maadhimisho haya ya kumbukumbu yanafanyika kwa mujibu wa mamlaka iliyotolewa na Baraza Kuu.