Yumkini hali ya mambo bado si shwari kwenye mji mkuu wa Libya, Tripoli ambako tangu kuzuka machafuko wiki iliyopita takriban raia 21 wameuawa wakiwemo wanawake na watoto huku 16 wakijeruhiwa. Sasa Umoja wa Mataifa watoa wito kwa pande kinzani kuwanusuru raia hao.
Machafuko yenye mwelekeo wa kijamii yanayoendelea katika jimbo la Mopti katikati mwa nchi ya Mali yanatia wasiwasi mkubwa kwa mujibu wa ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa.
Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani kwenye Umoja wa Mataifa, Jean-Pierre Lacroix amelihutubia Baraza la Usalama la umoja huo na kuliarifu hali ilivyo hivi sasa nchini Mali, hususan usalama.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani vikali mauaji ya waandamanaji huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC akisema kitendo hicho hakikubaliki.
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC watu sita wameuawa jumapili kwenye mji mkuu Kinshasa wakati wa maandamano yaliyoandaliwa na kanisa katoliki nchini humo. John Kibego na ripoti kamili.