Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, limetaka ulinzi zaidi kwa wafanyakazi wa kutoa misaada nchini Sudan Kusini kufuatia shambulizi la mwishoni mwa wiki lililofanywa na watu wenye silaha dhidi ya wafanyakazi wa kimataifa wa kusambaza misaada.