Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Afrika Magharibi ,UNOWAS, Mohamed Ibn Chambas, amelaani vitendo vya ghasia viliyofanyika kwenye maeneo tofauti tofauti nchini Senegal ambako mtu mmoja ameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa.