Wataalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wameonyesha wasiwasi wao kufuatia msako unaofanyika dhidi ya waandamanaji nchini Cameroon, baada ya Rais Paul Biya kuchaguliwa tena kuongoza nchi hiyo, hivyo wametaka uhuru wa kujieleza, kukusanyika kwa amani pamoja na uhuru wa kujiunga kwenye vikundi uheshimiwe.