Chuja:

Lesvos

UNICEF/Pavlos Avagianos

UNHCR yajenga mahema kunusuru wakimbizi baada ya kambi ya Moria kuteketea kwa moto,

Hatimaye mamia ya wasaka hifadhi kwenye kambi ya Moria iliyoteketetea kwa moto katika kisiwa cha Lesvos nchini Ugiriki wiki iliyopita, sasa wamepata makazi kwenye mahema yaliyosimikwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR. Ahimidiwe Olotu na taarifa kwa kina.

UNHCR inasema kuwa takribani wasaka hifadhi 2,200 wamepatiwa malazi kwenye eneo la dharura ambapo shirika hilo limesimika mahema 280.

Sauti
2'10"
IOM/Amanda Nero

UNHCR yasema hata baada ya kuvuka baharí ya Mediteranea bado maisha ni shubiri kwa wakimbizi

Huko nchini Ugiriki, maisha yamezidi kuwa ya shubiri kwa wakimbizi na wasaka hifadhi waishio kwenye kambi  ya muda ya Moria kisiwani Lesvos, wakati huu ambapo wanaishi watu elfu 10 katika eneo lililokuwa limeandaliwa kuhifadhi watu elfu 3. Anold Kayanda na ripoti kamili.

(Taarifa ya Anold Kayanda)

Nats..

Kambini Moria kisiwani Lesvos nchini Ugiriki, wakimbizi na wasaka hifadhi, wake kwa waume, vijana na watoto wakiendelea na shughuli zao katika mazingira magumu kupita kiasi, makazi yao yakiwa yameezekwa kwa karatasi za nailoni.

Sauti
1'51"