Mwalimu wa hisabati ageukia ujasiriamali Lesotho
Benki ya Dunia kupitia miradi mbalimbali imekuwa mstari wa kuchagiza maendeleo ya wananchi katika nchi zinazoendelea. Miongoni mwa wanufaika iwe mijini au vijijini ni wanawake ambao kupitia miradi hiyo hupatiwa mafunzo ikiwemo ya ujasiriamali. Sambamba na mafunzo hupatiwa mikopo ili kuweza kutekeleza kwa vitendo mafunzo waliyopatiwa ili hatimaye wajikwamue na umasikini.