Mwakilshi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC Leila Zerrougui amepongeza ukomavu wa raia wa nchi hiyo uliofanikisha uchaguzi mkuu nchini humo na hatimaye Rais mpya Felix Tshisekedi kuapishwa na kuanza rasmi awam yake ya uongozi wiki iliyopita.