Law, crime

Wasomalia 57 wafariki dunia baada ya kuzama kwenye pwani ya Yemen

Kiasi cha watu 57 raia wa Somalia wamerafiki dunia baada ya boti waliokuwa wakisafiria kuzama maji katika pwani ya Yemen.

KM Ban awalaani maharamia wa Somalia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema amevunjwa moyo na

kusikitishwa kufuatia ripoti za mauwaji kwa raia wanne wa kimarekani waliotekwa

na maharamia katika pwani ya Somalia.

Wahamiaji wa Libya wakimbia mapigano

Wahamiaji kutoka Libya wameanza kuvuka mipaka na baadhi yao wameripotiwa kupiga

hodi nchini Tunisia wakijaribu kusaka hifadhi kutokana na machafuko

yanayoendelea katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.

Baraza la haki za binadamu kuijadili Libya

Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa linakutana wiki hii kujadilia

mwenendo wa mambo huko Libya. Mkutano huo ni matokoe ya maombi yaliyowasishwa na Hungary kwa Umoja wa Ulaya na tayari umeungwa mkono na nchi wanachama 44.

Baraza la usalama la laani matumizi ya nguvu kudhibiti maandamano Libya

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limetoa wito wa kumalizwa haraka kwa

ghasia nchini Libya na kulaani hatua ya serikali ya nchi hiyo jinsi

ilivyopambana na waandamanaji wa upinzani.

Navi Pillay ashutumu matumizi ya nguvu kwa waandamanaji wa Libya

Kamishna wa Umoja wa Mataifa anayehusika na haki za binadamu Navi Pillay ameonya juu ya matumizi ya nguvu nchini Libya kujaribu kuzuia maandamano ya amani akisema kuwa hatua hiyo inaweza kupindukia haki za kibinadmu.

Askari 9 wa DRC wafungwa kutokana na ubakaji

Mahakama moja ya kijeshi nchini Congo imewatupa gerezani askari 8 ambao wamepatikana na hatia ya kuhusika kwenye tukio la ubakaji wa wanawake 50 katika eneo kaskazini mwa nchi hiyo.

UM waanzisha polisi maalumu kuwalinda wanawake Afrika ya kati

Umoja wa Mataifa umeanzisha wataalamu wa usalama ambao watajishughulisha na utoaji wa huduma za usamaria mwema, lakini wakijikita zaidi kwenye maeneo ya kuwalinda wanawake wakimbizi.

UM wakabidhi rasmi shughuli za ulinzi za mahakama kwa Sierra Leone

Timu ya Umoja wa Mataifa inayohusika na ulinzi wa amani katika mahakama maalumu nchini Sierra Leone imekabidhi majukumu yake ya ulinzi na usalam kwa serikali ya nchi hiyo.

Kiongozi wa UM nchini Kosovo atoa wito kuwepo na uchunguzi kutokana na tuhuma za biashara ya viungu vya binadamu

Kiongozi wa Umoja wa Mataifa nchini Kosovo jana ametoa wito wa kuwepo na uchunguzi wa haraka kuhusu tuhuma kwamba wafuasi wa kundi la KLA, Kosovo Liberation Army walijihusisha na biashara ya viungu vya binadamu katika mwaka 1999 wakati wa mapambano dhidi ya Waserbia na jeshi la Yugoslavia.