Law, crime

Mfuko wa UM kupambana na uharamia kupata dola milioni 5

Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa kupambana na uharamia pwani ya Somalia umeahidiwa dola zaidi ya milioni 5 katika siku ya mwisho ya mkutano wa kupambana na uharamia uliokamilika mjini Dubai.

Mashambulizi Misrata yaweza kuwa uhalifu wa kivita:Pillay

Kamishna mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay leo amelaani vikali matumizi mabomu mtawanyiko na silaha nzito zinazotumiwa na majeshi ya serikali Libya kwa lengo la kuchukua udhibiti wa mji wa Misrata.

Juhudi za kimataifa zinahitajika kukabili uharamia:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo ametoa wito wa kuwepo na juhudi za kina kupambana na uharamia kwenye pwani ya Somalia, akisema hali hiyo ni matokeo ya ukosefu wa usalama, kutokuwepo na serikali imara na umasikini kwenye taifa hilo la pembe ya Afrika.

Kilimo cha kasumba kupungua Afghanistan 2011:UNODC

Kilimo cha kasumbu kinatarajiwa kupungua kwa mwaka huu wa 2011 nchini Afghanistan licha ya bei ya juu ya zao hilo imesema ripoti ya utafiti iliyotolewa leo na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya madawa na uhalifu UNODC.

Hakuna msamaha kwa ukatili wa kimapenzi:Wallstrom

Baraza la usalama limetakiwa kuhakikisha kwamba wanaotekeleza ukatili wa kimapenzi kama ubakaji hawapewi msamaha katika makubaliano yoyote ya kusitisha mapigano Libya au ivory Coast.

Pillay ashangazwa na mauaji yanayoendelea Syria

Mkuu wa tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Navi Pillay ameeelezea kushangazwa kwake kufuatia kuendelea kuripotiwa visa vya mauaji ya waandamanaji na vikosi vya usalama nchini Syria.

Wataalamu wateuliwa kuchunguza ukiukwaji haki Ivory Coast

Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limewateua wataalamu watatu ambao watachunguza madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Ivory Coast kufuatia ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi wa urais uliokumbwa na utata.

Utawala wa sheria muhimu kujenga amani ya jamii:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa leo amesisitiza haja ya haraka ya kuimarisha utawala wa sheria duniani,akisema unaweza kusaidia kukabiliana na baadhi ya changamoto zinazoikabili jumuiya ya kimataifa hivi sasa.

Baraza la usalama lapitisha azimio kukabili uharamia Somalia

Kwa kutambua haja ya hatua zaidi za kupambana uharamia, leo baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeamua kufikiria hatua za haraka za kuanzisha mahakama maalumu Somalia za kuwafungulia mashitaka na kuwahukumu maharamia Somalia na ukanda mzima.

Dhulma za mtandao dhidi ya watoto zidhibitiwe:UNODC

Afisa wa Umoja wa Mataifa leo ameonya kwamba dhuluma kwa njia ya mtandao dhidi ya watoto zinaongezeka hasa kwa kuwa watu wengi zaidi sasa wanapata fursa ya kutumia internet.